Klein Calvin
Member
- Dec 18, 2017
- 6
- 0
Hivi ukifungiwa maisha na tff usishiriki masuala yoyote ya soka ni mambo yepi hasa inatakiwa usifanye? Na je ikitokea bado huyo mtu akaendelea kufanya mambo fulani ya michezo ni hatua zipi zitachukuliwa na tff dhidi ya mtu huyo? Huyo mtu mfano anaweza akagombea ubunge au akateuliwa na rais kuwa mbunge na kisha rais akamteua kuwa waziri wa michezo, vipi hapo sheria za tff zinasemaje? Na mwisho hizi adhabu za kumfungia mtu asijihusishe na soka maisha haikidhani na katiba mama ya nchi ya mtu kuwa huru ndani ya nchi yake na kwa kuwa chombo pekee cha kutoa hukumu ni mahakama? Msaada kwa wataalam wa haya.