Adhabu za kufungiwa kutojihusisha na soka maisha

Klein Calvin

Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
6
Reaction score
0
Hivi ukifungiwa maisha na TFF usishiriki masuala yoyote ya soka ni mambo yepi hasa inatakiwa usifanye? Na je ikitokea bado huyo mtu akaendelea kufanya mambo fulani ya michezo ni hatua zipi zitachukuliwa na TFF dhidi ya mtu huyo?

Huyo mtu mfano anaweza akagombea Ubunge au akateuliwa na rais kuwa mbunge na kisha rais akamteua kuwa waziri wa michezo, vipi hapo sheria za TFF zinasemaje?

Na mwisho hizi adhabu za kumfungia mtu asijihusishe na soka maisha haikinzani na katiba mama ya nchi ya mtu kuwa huru ndani ya nchi yake na kwa kuwa chombo pekee cha kutoa hukumu ni mahakama? Msaada kwa wataalam wa haya.
 
wanamaanisha yani Wambura asikanyage hata uwanja wa taifa kutazama mechi yoyote ya mpira wa miguu.
 
Hii hukumu imekaa kichuki chuki zaidi........mtuhumiwa ana haki ya msingi ya kusikilizwa ...wana sheria wanaweza kutujuza zaidi hapa.......
 
wambura sijui kwanini ana mkosi na uongozi wa mpira nchi hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…