Adhabu za TanRoad,Traffic,Sumatra ni double standard katika serikali moja!

Adhabu za TanRoad,Traffic,Sumatra ni double standard katika serikali moja!

KakaKiiza

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,794
Reaction score
9,075
TANROADS, SUMATRA, TRAFFIC, ADHABU YA SPIDI HAIKUBALIKI KABISA.

Waraka wa BASHIR YAKUB
+255784482959.

Traffic 30,000, Sumatra 80,000, Tanroads 90,000 =200,000 Tshs. Ni adhabu ya kosa moja tu la kukiuka spidi iliyokubaliwa.Ni taarifa iliyoenea mtandaoni kwa sasa. Ni kuwa kosa moja tu la spidi kila mamlaka kati ya hizo hapo juu itakutoza faini iliyoainishwa.

Binafsi nimeshuhudia risiti ya malipo ya Tanroads ikiwa imetoza kiwango hicho. SWALI ni kama jambo hilo linakubalika kisheria.

1. DOUBLE JEOPARDY.

Hii ni kanuni kati ya kanuni za kisheria za Misingi ya Haki za Asili "Principle of Natural Justice". Ni kanuni inayokataza kabisa kabisa kosa moja kuadhibiwa zaidi ya mara moja.

Tuone DUNIA inasemaje kuhusu Double jeopardy.

a ) HAPA TANZANIA.

Kifungu cha 21 cha Kanuni za Adhabu (Penal Code) kinasema kuwa mtu hataadhibiwa mara mbili au zaidi kwa kosa moja alilofanya chini ya Sheria yoyote.

Maana ya maneno "Sheria yoyote" ktk hicho kifungu ni kuwa, iwe ya usalama barabarani, ya Tanroads au Sumatra , mtu akishaadhibiwa kwa sheria mojawapo kati ya hizo inatosha.Ni mara moja tu.

Pili, Sheria ya Tafsiri za Sheria(The Interpretation of Laws Act), Sura ya kwanza , kifungu cha 70 kinasema, ............. kwa kosa moja, mtu ataadhibiwa mara moja tu.

b ). AFRIKA MASHARIKI.

Kenya. Katiba yao ibara ya 50(2)(o) inasema kuwa itakuwa ni makosa chini ya katiba na Sheria nyingine kwa mtu kuadhibiwa zaidi ya maramoja kwa kosa moja. Ibara hii inasomwa na Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Jinai vifungu vya 138- 142 .

Uganda. Kanuni za Adhabu , kifungu cha 21 kinasema kuwa kwa kila kosa , mtenda kosa ataadhibiwa mara moja tu.

C ) . AMERIKA.

Usa. Katika kesi ya Bentom vs Maryland, 395, US 784(1969), mahakama ya juu iliitaja "double jeopardy" yaani mtu kuadhibiwa mara mbili au zaidi kwa kosa moja kama ukandamizaji wa kiwango cha juu kabisa wa haki.

d ). UMOJA WA ULAYA.

Mkataba wa Umoja wa Ulaya wa Haki za binadamu( European Convention on Human Rights) , Ibara ya 4 inasema kuwa, hakuna mtu akayeadhibiwa na dola kwa kosa ambalo tayari ameshakutwa nalo hatia na kutumikia adhabu ya kosa hilo.

e ). MKATABA WA KIMATAIFA WA HAKI ZA KISIASA NA KIRAIA.

Unaitwa "International Covenant on Civil and Political Rights". Tanzania imesaini mkataba huu. Ibara yake ya 14(7) inasema kuwa, hakuna mtu atakayeadhibiwa tena kwa kosa lilelile baada ya kuwa ameadhibiwa kwa taratibu za kisheria za nchi yake.

2. MAKOSA KATIKA ADHABU HII.

Adhabu tatu si tu kosa la kawaida bali pia lililokiuka kabisa kabisa haki za binadamu. Kwa namna yoyote ilivyo kosa moja katu haliwezi kuadhibiwa mara tatu na mamlaka tatu tofauti. Abadan

Sheria zote za ndani na zile za kimataifa zimekataa na sisi pia hatutakubali. Double jeopardy ni kosa duniani kote na Tanzania.

Tunakemea mwendo kasi na mwendo uliokiuka taratibu za barabara husika, lakini tunakemea zaidi ukiukwaji wa sheria na haki za binadamu katika kushughulikia jambo hilo.

3. NASAHA

Lazima iwepo adhabu moja inayotolewa na mamlaka moja. Na adhabu hiyo iwe ya kukadirika(reasonable) na sio ya kukomoa au kulenga kuongeza mapato ya mamlaka/biashara.

Tumezoea ile ya 30,000 ya traffick nadhani inatosha na ni ya kukadirika. Pia imesaidia sana kwani sasa vibao vya spidi vinazingatiwa sana na madereva.

Inawezakana Tanroads na Sumatra mna mpangio wa kuongeza makusanyo/mapato. Na iwe hivyo lakini sio kwa kuvunja Sheria na kuonea Watanzania. Hili hatutakubali.



Samsung SH 8 Mobile Traveller
 

Attachments

  • Tanroad.jpeg
    Tanroad.jpeg
    95.3 KB · Views: 70
Kama hiyo taarifa ni sahihi basi huo ni uonevu uliopita kiasi, 200k kwa hali ya sasa hivi🙁😵
 
Uzuri wetu sisi wadanganyika ni kuwa kila mtu ataonesha kuhudhunishwa na hili kwa maandishi hapa, ku-quote vifungu vya sheria n.k Kuna watu wana taaluma ya sheria na tena wana vyama vyao ambavyo vinaweka viwango vya kulipwa na isiwe chini ya hapo kwa wanasheria wote, yaani maslahi yao binafsi....walipotaka kufuta chama chao walianza kampeni ooooh wadanganyika msikie jinsi tunavyoonewa, LEO wadanganyika wanaonewa, wako kimya.

Hutasikia imefunguliwa kesi ya kikatiba kupinga hili, ila ngoja posho zifutwe......si zinagusa matumbo yao! Na wakijua wao hawatakaa wapigwe hizo faini na ikitokea basi ubavu wa kulipa wanao; mimi nimenunua passo ilu kukwepa kuingia filling station mara kwa mara, tzs 20,000 kwa wiki, wewe unataka budget ya wiki kumi kwa kosa moja tena ukutwe nimebambikwa.

ULITAKA TUFANYEJE?.....SIO SWALI!!!!!
 
Asante. Mimi nilitaka kuanzisha thread kuwauliza hawa TLS. Je ni sahihi kosa moja kuadhibiwa mara tatu? Yaani unahukumiwa na polisi,sumatra,tanroads?
 
Uzuri wetu sisi wadanganyika ni kuwa kila mtu ataonesha kuhudhunishwa na hili kwa maandishi hapa, ku-quote vifungu vya sheria n.k Kuna watu wana taaluma ya sheria na tena wana vyama vyao ambavyo vinaweka viwango vya kulipwa na isiwe chini ya hapo kwa wanasheria wote, yaani maslahi yao binafsi....walipotaka kufuta chama chao walianza kampeni ooooh wadanganyika msikie jinsi tunavyoonewa, LEO wadanganyika wanaonewa, wako kimya.

Hutasikia imefunguliwa kesi ya kikatiba kupinga hili, ila ngoja posho zifutwe......si zinagusa matumbo yao! Na wakijua wao hawatakaa wapigwe hizo faini na ikitokea basi ubavu wa kulipa wanao; mimi nimenunua passo ilu kukwepa kuingia filling station mara kwa mara, tzs 20,000 kwa wiki, wewe unataka budget ya wiki kumi kwa kosa moja tena ukutwe nimebambikwa.

ULITAKA TUFANYEJE?.....SIO SWALI!!!!!


Hizo ni sheria zilishapitiswa na bunge kwahiyo unataka kina Lissu wafanyaje kwa mfano ? Hata wakifungua kesi kama ni agizo toka juu haitasaidia chochote, jambo la msingi ni kuwalilia hao wabunge wenu ambao ni wengi na wana uwezo wa kubadilisha hizo sheria bingeni kama walivyozipitisha kwa wingi wao
 
Tulizeni shanga,no. Isomeke mpk iwe infinity.
 
Subscribed... nitapitia baadae nikiwa home na glasi yangu ya maji. Kunywa maji kwa afya yako. Soda kemikali (bajet ya soda haisomi).
Anyways huu uzi nimeupenda sana
 
Hizo ni sheria zilishapitiswa na bunge kwahiyo unataka kina Lissu wafanyaje kwa mfano ? Hata wakifungua kesi kama ni agizo toka juu haitasaidia chochote, jambo la msingi ni kuwalilia hao wabunge wenu ambao ni wengi na wana uwezo wa kubadilisha hizo sheria bingeni kama walivyozipitisha kwa wingi wao
Polee kwa hamasa uliyopata mkuu, ila umenidhania tu......ULIPO SIPO.
 
Wapigwe tu hata mara kumi kwa kosa moja.
Kuna masheria ya hovyo tunayoiga toka kwa wazungu ili hali tunajua watu wetu wanatabia kama wendawazimu.

Kuna watu wanakwenda mwendo kasi bila kujali kabisa kuwa kuna watu wastaarabu wanaoweza kuathirika kwa ajali.

Tatizo hapa tumeangalia huruma kwa wavunja sheria na mafisadi bila kujali watu wema wanaoathirika.

Mtu amenunua gari hana hata mwezi na hajawahi kuwa dereva tangu amezaliwa lakini anaendesha rafu kama kichaa , matokeo yake anawasababishia ajali wasio na hatia na kuleta vifa. Hii sio sawa kuwatetea nadhani hata wanao watetea nao wapigwe marufuku na viNGOs Vyao vya kuhamasisha na kufariji na kuwapa ujasiri wavunja sheria.
Makosa ya barabarani ni madogo lakini yana athari mbaya sana kwa maishwa ya watu.

Nadhani ni vyema kabisa Polisi ,Sumatra na Tanroad wakajipanga barabarani ili ukichomoka polisi uangukie Sumatra,Ukichomoka Sumatra uangukie mikononi mwa Tanroad.
Nchi yenye watu wanaohubiri haki tu kwa wahalifu wa wazi bila kuwakataza inatengeneza na kuwapa nguvu wahalifu.

Makosa ya barabarani ni tofauti kabisa na jinai. Ndio maana dereva akigonga watu 10 na kufa kwa mwendo kasi anahukumiwa kwa kila mtu. Halafu tena anakuwa na mashitaka ya ziada kama kuendesha gari bila kujali na kuliharibu.
Kama lilikuwa bovu basi unaambiwa pia uliendesha gari bovu.

Kwa hiyo tusiwadanganye watu kuwa kuna double standard kwenye haya makosa yenye faini za hapo kwa hapo.

Serikali inapoweka sheria kali kwenye vyombo au vifaa vinavyoweza kuleta maafa makubwa kwa wakati mmoja wanafanya hivyo kwa manufaa ya umma sio mtu mmoja.

Gari linaweza muda wowote likaendesha na mlevi au mtu mwenye stress zake na kusababisha maafa makubwa na kuharibu mali za watu. Kwa hiyo ni lazima kila mamlaka iliyotoa leseni isimame kidete kuzuia hali hiyo.
Ikumbukwe kuwa dereva ni mtu ambaye anafanya kazi ya kuendesha gari kisheria kabisa na sio mhalifu ndio maana akawekewa mamlaka mbalimbali za kumdhibiti ili asije akasababisha madhara kwa kutumia chombo hicho.

Hata Maengineer,madaktari,manesi,Wahasibu na sasa wanasheria inabidi wawe na bodi za kufatilia mienendo na maadili ya kazi zao na ubora wa kazi zao ; lengo likiwa ni kudhibidi uharibifu na madhara yanayoweza yakasababishwa na utaalam wao. Nesi akigundulika kuwa ameua mtu kwa makusudi basi ataadhibiwa kwa kufukuzwa kazi, kunyanganywa leseni na kupelekwa mahakamani. Adhabu tatu hizo kwa kosa moja mana limefanywa na mtu mwenye taaluma hiyo halali na aliomba leseni ili atoe huduma bora a kwa uadilifu kwa jamii. Sasa anapoamua kukiuka kiapo au leseni yake ni lazima kila mamlaka iliyomruhusu kufanya kazi hiyo imshughulikie kwa mujibu wa kananuni walizomuonya na kumuelekeza tangu mwanzo alipokua anaomba leseni hiyo.

Kosa moja linaweza kupewa adhabu tofauti tofauti kulingana na sheria zilizopo.
Hata mahakamani unaweza ukahukumiwa miaka mitano na kulipa faini na viboko juu.
Hilo ni kosa moja lenye adhabu mchanganyiko kulingana na aina ya kosa.

Ninavyojua mimi ni kuwa kosa moja la mwendo kasi hauwezi kuhukumiwa na polisi mara mbili.
Yani umeendesha speed 180 kph kwenye msongamano wa watu bila sababu yoyote halafu polisi wakupige faini 20,000/- mara mbili kwa kosa hilo hilo.
Lakini unaweza ukapigwa faini ya polisi halafu pia kama una leseni ya sumatra iliyokupa masharti ya kudhibidi mwendo wa gari lako kwa kuweka kidhibiti mwendo na hauna hicho kifaa basi watakutwanga faini tena. Na Tanroad kama walikuambia kuwa barabara hiyo usiipite kwa mwendo zaid ya 50 watakutwanga pia bila wasiwasi na ni halali kabisa. Wakikuacha ndio watakuwa wamevunja sheria inayowataka wakuadhibu.

Wakati mwingine wale wenye taaluma ya sheria watumie taaluma yao kupunguza makosa kwa kuielimisha jamii umuhimu wa kufuata sheria , pamoja na ukweli kuwa makosa yanapoongezeka ndio ulaji wao unapoongezeka kwa kasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom