ndugu wana jf,kutokana na matokeo mabovu ya shule nyingi za sekondari wizara sasa imeamua kuleta mashuleni mabadiliko kadha wa kadha katika kile kinachoitwa big results,lakini ni onavyo mimi bado kuna tatizo la lugha ya kufundishia mashuleni,mathalani mtoto anafundishwa kwa miaka saba kwa lugha ya kiswahili kwa miaka saba au nane halafu mara ghafla tunabadilisha lugha na kuanza kutumia kiingereza mara mtoto anapoingia sekondari,je kweli mtoto aliyesoma shule zetu za kawaida anaweza kuelewa vema masomo??mimi naona ni tatizo na sababu ya watoto wengi hata kufeli katika mitihani yao ya mwisho,je nyie mna maoni gani??