adhari ya lugha ya kufundishia mashuleni

daffy

Senior Member
Joined
Aug 29, 2013
Posts
196
Reaction score
30
ndugu wana jf,kutokana na matokeo mabovu ya shule nyingi za sekondari wizara sasa imeamua kuleta mashuleni mabadiliko kadha wa kadha katika kile kinachoitwa big results,lakini ni onavyo mimi bado kuna tatizo la lugha ya kufundishia mashuleni,mathalani mtoto anafundishwa kwa miaka saba kwa lugha ya kiswahili kwa miaka saba au nane halafu mara ghafla tunabadilisha lugha na kuanza kutumia kiingereza mara mtoto anapoingia sekondari,je kweli mtoto aliyesoma shule zetu za kawaida anaweza kuelewa vema masomo??mimi naona ni tatizo na sababu ya watoto wengi hata kufeli katika mitihani yao ya mwisho,je nyie mna maoni gani??
 
Sidhani kama lugha ni kikwazo ndio maana hata kichwa cha habari umeandika adhari badala ya athari,ukiangalia kati ya masomo yaliyoongoza kwa kufelisha kiswahili kipo,kwahiyo lugha si sababu,kwa binafsi yangu naona tatizo lipo kwenye mtaala mzima wa masomo,walimu wenye sifa zinazotakiwa,vifaa vya kufundishia kwa vitendo na kuwathamini walimu ili wajitolee kwa japo %75 mengine ni propaganda na siasa
 
Sidanganyiki mtoto wangu atasoma kwa lugha ya kiingereza kuanzia kindergaten!Waajiri wote wanatumia kiingereza,swahili ni kudanganyana
 
Kufaulu au kufeli hakuhusiani na lugha japokuwa ndio lugha inachangia wanafunzi wengi kufanya vibaya, kwani lugha gani inatumika shule za msingi? na bado mbona huko huko wanashindwa fanya vizuri japokuwa inayotumika ni lugha mama tazama wanaokwenda kidato cha kwanza ufaulu wao kwa sasa utachoka mi nadhani ni misingi mibovu tu binafsi ambayo asilimia kubwa haichangiwi na lugha peke yake ndio lugha uja baadaye o level nakuendelea kuongezea ubovu sikatai.
 
Ni adhari au athari? Ndio hiyo lugha unayozungumzia au nyingine?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…