Adidas yafanya mazungumzo na Kanye West kuhusu mauzo ya bidhaa zilizokwama kuuzika

Adidas yafanya mazungumzo na Kanye West kuhusu mauzo ya bidhaa zilizokwama kuuzika

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Rapa na Mfanyabiashara #YE na kampuni ya kuunda Mavazi ya #Adidas wanaripotiwa kufanya mazungumzo ya kurudisha ushirikiano ikiwa ni miezi michache tangu kuvunjika kwa mkataba wao baada ya Kanye kutoa kauli zilizoonesha ubaguzi wa rangi.

Mazungumzo hayo yanatarajiwa kurejesha mauzo ya bidhaa za Adidas zenye thamani ya Tsh. Trilioni 3 zilizokwama kuuzika baada ya kuvunjika kwa mkabata wao. Pia, kubadili baadhi ya vipengele vya umiliki wa biashara hiyo.

Licha ya Adidas kushindwa kuuza bidhaa zilizobuniwa na #KanyeWest, Rapa na Mfanyabiashara huyo naye alipata hasara ya kupoteza dili la Tsh. Trilioni 4.6 kutokana na kauli zilizoonesha Ubaguzi dhidi ya #Wayahudi.

Untitled.png
WEALTH
 
Wayamalize ,atakua amejifunza ,sio Kila kinachokuja mdomoni cha kuongea
Ye namuelewa Sana..ameshajua kucheza na hwa maboya..aliona wanampiga akawatekenya wakajaa.

Niambie ni nani tokea ulimwengu uumbwe alishawahi vunja mikataba na makampuni makubwa Bila ya kesi na kupotezwa.

Jamaa ni genius na atawapeleka puta..ana confidence ya ajabu sijawahi ona
 
Kanye amekua maji wasipoyanywa watayaoga
Hi hi ndio kitu Cha msingi kwenye maisha ya Sasa hivi..mfano mzuri wafanyakazi makazini..kuna ambao wakitaka kuondoka ,hr wanawaita mezani Wana counter offer...kuna wengine ukiagwa unaambiwa safari njema.

Kuna wengine ukiagwa wanakuchukulia poa wanakuaga ila baada ya muda wanaona pengo lako ..wanakuomba tena urejee, Kanye yupo kundi la mwisho.

Alihakikisha product zake ndio zinabeba hizi kampuni kiasi ya kwamba akiondoka watakula hasara ya ajabu ..
Na kweli Jamaa kagusa penyewe mikataba ikavunjwa kimihemko..mwisho wa siku wanamwita mezani with new teerms
 
Kanye amekua maji wasipoyanywa watayaoga
Yani Kuna kipindi nilikuwa napita kwenye msongo mkubwa sana wa mawazo, nilikuwa na stress balaaa...lkn wewe uliniponya nikawa busy na kufatilia ule Uzi wa isidingo...Yani ulinisaidia,, Hadi Leo hua nakuheshimu....nakupa maua yako mapema
 
Waaaow Asante sana mkuu. Barikiwa zaidi.
Yani Kuna kipindi nilikuwa napita kwenye msongo mkubwa sana wa mawazo, nilikuwa na stress balaaa...lkn wewe uliniponya nikawa busy na kufatilia ule Uzi wa isidingo...Yani ulinisaidia,, Hadi Leo hua nakuheshimu....nakupa maua yako mapema
 
Adidas biashara ngumu sana kwao hasa ya jezi hizi jezi zao saiv mtu mwenye kitambi havai tayari washatukosa ukiangalia kwenye list ya jezi kali utagundua ni za puma zinavalika na watu yupe yote sio mijezi ya adidas ukivaa unaonekana umebinuka
 
Back
Top Bottom