Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Adinani Hussein hajapatikana licha ya Polisi kupokea Tsh 13 Million kutoka kwa ndugu

Stuxnet

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2011
Posts
13,417
Reaction score
23,310
Kutoka Ukurasa wa Boniface Jacob Mtandao wa X: SIKU 280 TANGU APOTEE ADINANI HUSSEIN MBEZI MIKONONI MWA POLISI

Maarufu kama (ADAM),umri wa miaka 32,mkazi wa Kinyerezi,mtaa wa Faru,Jimbo la Segerea,Baba wa watoto wanne.

1. Adinan Hussein Mbezi alipotea tarehe 12 September 2023 alipokuwa safarini Mwanza

2. Adinani Hussein Mbezi alizaliwa mwaka 1992 ni mfanyabiashara anaye miliki vituo 11 vya kuoshea magari Dar es saalam vya "ONE TOUCH" Pia ni mwanasiasa ambaye alishawahi kuwa CCM baadae akagombea udiwani kupitia ACT WAZALENDO uchaguzi wa 2020 kata ya Yombo Vituka.

3. Tarehe 12 September 2013 ADINANI alipiga simu kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE kumtaarifu kuwa amekamatwa na Polisi,kwamba wapo njiani kurudi Dar es saalam atamjulisha kituo watakacho mpeleka baada ya kufika Dar es saalam.

4. Tarehe 19 September 2023 ADINANI alipiga simu kwa Mama yake mlezi anayeishi maeneo ya ZOO,Chanika,Dar es saalam kwa kupitia namba ya simu 0659167082

Akimueleza Mama yake kuwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika kituo cha Polisi cha Tazara,akaomba Mama yake amsaidie kumpatia namba ya Kaka yake aitwaye SAMIR HUSSEIN MBEZI

Pia aliomba Mama yake ampe taarifa rafiki yake aitwaye AMIR KHALID NASIBU (SAM) mwenye namba za simu 0711959432
ambaye amekuwa akishirikiana na familia katika kumfuatilia ADINANI kwa kila hatua.

5. ADINANI alijitahidi sana kufanya mawasiliano na ndugu zake kila kituo alichokuwa anapelekwa Jijini Dar es saalam tangu akamatwe Mwanza.

Alipiga simu akiwa Central Police Station,alipiga simu akiwa Kituo cha polisi Stakishari na simu ya mwisho alipiga kwa mke wake ROSEMERRY MASSAWE akiwa Tazara kupitia simu ya Polisi nambari 0659167082

Sasa akimtaarifu mke wake kuwa amepigwa sana,anahali mbaya ambayo mke wake aligundua hali ya mme wake kuwa yupo katika mateso

ADINANI aliomba mke wake atume kiasi cha Shillingi laki 5 katika namba 0659167082 ambayo alisema namba ya simu ya Polisi aliyekuwa naye wakati huo,kwa ahadi ya kiasi hicho kingesaidia asiendelee kuteswa zaidi.

Mke wake ROSEMERRY MASSAWE alitekeleza ombi la mume wake kwa kutuma laki tano.

6. Ndugu wa ADINANI walifika kituo cha Polisi Tazara,ambapo afande Kaduma mwenye namba 0757078736 alikana kumshikilia ADINANI kituo cha Tazara

Mwisho walienda Kituo cha Polisi Oysterbay ambapo walielekezwa waende Kituo cha polisi kati ofisi ya ZCO kandaa maalum DSM,kumuuliza Afande Mafwele kuhusu ndugu yao kushikiliwa na Polisi

ZCO Mafwele alikana kumshikilia ADINANI,aliwatolea orodha ya mahabusu wanaoshikiliwa kituoni pale, Jina la ndugu yao halikuwemo katika orodha ya mahabusu.

Pia aliwataarifu kuwa na wao Kanda maalum ya Dar es saalam wanamtafuta ADINANI kama mtuhumiwa,wakimpata wataitaarifu familia yake.

7. Ndugu wa ADINANI katika kumtafuta ndugu yao walifanikiwa kuonana na Kigogo mmoja wa Jeshi la Polisi,ambaye aliwathibitishia kuwa ndugu yao yupo Kituo cha Polisi Tazara,aliomba kiasi cha shillingi million 10 ilikuwasaidia kumaliza sakata la ndugu yao,

Ndugu walitoa kiasi cha shillingi million 10 kupitia dereva wake,lakini baada ya kutoa kiasi hicho,Kigogo huyo aligeuka kuwapa jibu kumbe ni majina tu ndiyo yanafanana,lakini ndugu yenu hayupo kituo cha polisi Tazara

8. Baada ya siku kadhaa kupita ndugu wa ADINANI walipigiwa simu na mtu aliyejitambulisha ni Askari wa Kituo cha polisi Mburahati kupitia namba ya simu 0713440820

Askari huyo aliwaeleza Kuwa ADINANI yupo Kituo cha Polisi Mburahati na hali yake ni mbaya sana.
Askari huyo aliomba watumiwe kiasi cha Millioni 2 na laki 5 ili wasiendelee kumuadhibu na kumpa mateso ndugu yao.

Ndugu walipotuma shillingi million mbili na laki tano simu hiyo haikuwahi kupatikana tena.

9. ADINANI alikuwa na mpenzi wake mwingine Dodoma,ADINANI alimpigia mpenzi wake huyo kumjulisha kuwa amekamatwa na Polisi na kumtaarifu kuwa kama anamtafuta amtafute kupitia rafiki yake mwenye namba 0742866092

Alipompigia mtu huyo alikata simu ya kawaida akapiga video call na kuwataarifu ADINANI hayupo tena Duniani

10. Gari ya ADINANI yenye usajili T146 DPY imeonekana kituo cha Polisi Selander bridge.


20240713_093150.jpg
 
siku yaja watalia na kusaga meno wakitamani siku zirudi nyuma wasitende waliyoyatenda ila haitawezekana

Kiburi cha mtu ni uzima, mali na madaraka ila vyote huisha.

Siku ghadhabu ikiwaka juu ya hao watu risasi haijawahi kutuliza wala kuogofya!

Binadam mtu hatari sana anakuwa anakuchora tu.
 
Sababu kadhaa zinaweza kueleza kwa nini serikali za ubabe zipo sana Afrika:

  1. Historia ya Ukoloni: Nchi nyingi za Afrika zilikoloniwa na mataifa ya Ulaya na baada ya kupata uhuru, mara nyingi ziliachiwa mifumo ya kisiasa isiyo imara. Viongozi waliopata madaraka walitumia mifumo hiyo kujenga utawala wa kiimla.
  2. Ukosefu wa Taasisi Imara: Taasisi za kidemokrasia kama vile mahakama huru, vyombo vya habari vya kujitegemea, na vyama vya siasa vingi hazijajengwa imara katika nchi nyingi za Afrika. Hii inawapa nafasi viongozi wa kiimla kudhibiti madaraka.
  3. Umasikini na Ukosefu wa Elimu: Umasikini na ukosefu wa elimu vinaweza kuwafanya wananchi kutokuwa na uwezo wa kupinga serikali za kiimla au kushiriki kikamilifu katika mchakato wa kisiasa. Hii inaleta mazingira mazuri kwa viongozi wenye ubabe kujijenga na kudumu madarakani.
  4. Migogoro na Vita vya Ndani: Nchi nyingi za Afrika zimepitia migogoro ya kivita na vita vya wenyewe kwa wenyewe. Katika mazingira haya, viongozi wenye nguvu za kijeshi mara nyingi hupata nafasi ya kuchukua madaraka na kuendeleza utawala wa kiimla kwa kisingizio cha kudumisha amani na utulivu.
  5. Ukosefu wa Uwajibikaji: Katika baadhi ya nchi za Afrika, kuna ukosefu wa uwajibikaji kwa viongozi wa kisiasa. Hii inamaanisha kuwa viongozi wanaweza kufanya maamuzi ya kiimla bila kuogopa hatua za kisheria au kuondolewa madarakani.
  6. Ushawishi wa Nchi za Nje: Mataifa yenye nguvu za kiuchumi na kijeshi yamekuwa na ushawishi mkubwa barani Afrika. Wakati mwingine, mataifa haya yanaunga mkono viongozi wa kiimla ili kulinda maslahi yao ya kiuchumi na kisiasa katika eneo hilo.
 
Serikali yenye ubabe wa madaraka inaweza kufikia hatua ya kuteka watu wanaopinga utawala kwa sababu kadhaa:

  1. Kulinda Mamlaka: Serikali ya aina hii ina hofu ya kupoteza udhibiti na mamlaka yake. Inaweza kuona wapinzani kama tishio kwa utawala wao, hivyo hutumia vitisho na nguvu kuwanyamazisha.
  2. Kuzuia Harakati za Upinzani: Kuteka watu wanaopinga utawala ni njia ya kutisha na kuzuia watu wengine kujiunga na harakati za upinzani. Kwa kuwafunga au kuwatesa wapinzani, serikali inajaribu kudhoofisha na kuvuruga harakati za upinzani.
  3. Kusambaza Hofu: Kitendo cha kuteka wapinzani kinaweza kusababisha hofu miongoni mwa wananchi. Watu wanaweza kuogopa kusema au kushiriki katika shughuli za kisiasa zinazopinga serikali, hivyo kubaki kimya na kuacha serikali iendelee na utawala wake bila pingamizi.
  4. Kudhibiti Habari: Katika serikali za ubabe, uhuru wa vyombo vya habari mara nyingi hudhibitiwa. Kwa kuteka wapinzani, serikali inaweza kuzuia taarifa muhimu na maoni mbadala kusambaa kwa urahisi, hivyo kuwafanya watu wengi kuwa na mtazamo mmoja tu wa serikali.
  5. Kulinda Maslahi ya Kibinafsi: Viongozi wa serikali ya ubabe mara nyingi hutumia madaraka yao kwa manufaa ya kibinafsi na kundi dogo la watu wanaowazunguka. Wanaweza kuteka wapinzani ili kulinda maslahi yao binafsi na kuhakikisha kuwa hakuna mtu anayefichua ufisadi na vitendo vingine vya kihalifu wanavyofanya.
 
Intelegensia inanituma hivi, hapa kuna kisasi, hasa hasa, " Sio kangangania mke wa mtu mwenye wadhifa mkubwa kweli?, sio kila issue ni ya kisiasa yapo ya visasi kwa wenye nyadhifa zao!
-Siku hizi watu hawasemi tena utanijua mimi nani?, zama zimegeuka na kuwa Action! 😈
 
Intelegensia inanituma hivi, hapa kuna kisasi, hasa hasa, " Sio kangangania mke wa mtu mwenye wadhifa mkubwa kweli?, sio kila issue ni ya kisiasa yapo ya visasi kwa wenye nyadhifa zao!
-Siku hizi watu hawasemi tena utanijua mimi nani?, zama zimegeuka na kuwa Action! 😈
Una akili finyu
 
Intelegensia inanituma hivi, hapa kuna kisasi, hasa hasa, " Sio kangangania mke wa mtu mwenye wadhifa mkubwa kweli?, sio kila issue ni ya kisiasa yapo ya visasi kwa wenye nyadhifa zao!
-Siku hizi watu hawasemi tena utanijua mimi nani?, zama zimegeuka na kuwa Action! 😈
embu fanya wewe kesho sio mbali washakukamata. ujiulizi tu mbona umekuwa kama muriro unaojiwa unaruka ruka unaambiwa ostabey kuna kala kana alafu wewe unasema kuna uwanja mpira
 
Back
Top Bottom