Papaa Mobimba
JF-Expert Member
- Jan 27, 2018
- 882
- 3,337
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu akizungumza na wanahabari leo Januari 15 Makao Makuu ya chama hicho Magomeni Dar Es Salaam amesema “Wakitokea watu wanataka kujiunga ACT Wazalendo kutokea CHADEMA tutawapokea na tunawakaribisha sana kwa mikono miwili kwa sababu biashara ya chama cha siasa ni wanachama kwa hiyo kitakuwa ni chama cha ajabu tukisema hatutawapokea wanachama …narudia kusema tena ACT Wazalendo ipo tayari kuwapokea wapiganaji wote ambao wamekata tamaa wamechoshwa wamefadhaishwa kwenye vyama vyao kama umechoshwa na CHADEMA, ACT Wazalendo inakukaribisha kwa mikono miwili ukichoshwa na CCM, ACT Wazalendo ndio nyumbani, ukichoshwa na CUF njoo ACT Wazalendo”