Adui mkubwa wa afya ni vyakula vya kununua, pamoja na tamaa ya faida inalisha watu vibudu, mchele ulioharibika

round kick

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2025
Posts
345
Reaction score
1,145
Kuanzia matatizo ya vidonda vya tumbo, vijana kuwahi kuzeeka, kukosa nguvu za kiume, n.k. kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kula vyakula vya kununua

Kuna wafanyabiashara wa vyakula wao ni faida mbele, afya yako haina kipaumbele, wewe utalishwa vibovu wao watajipikia chakula tofauti.

Njia za kuweza kufaidika ni kama zifuatazo

  • Kununua nyama ya mnyama aliekufa, mgonjwa, n.k. nyama hizi ni bei rahisi zaidi
  • kwenda kuokota mizoga iliyotupwa, hasa kuku
  • kutumia mafuta ya transfoma kukaangia, yanatumika kwa muda mrefu sana.
  • kutumia mafuta yaliyo expire, ukiyaona kwenye kaangio huwa yana rangi nyeusi au brown
  • kwenda kuokota vyakula vilivyoharibika hasa mchele na kuupepeta upya
  • Kutumia nyanya, nazi na viungo vya viwandani badala ya viungo asili
  • n.k.
Usicheze na afya yako kwenye suala la chakula kuwa makini sana,ni heri ugharamike zaidi uwe unarudi kwako kula, kubeba chakula chako, kuletewa, n.k.
 
Bora uuziwe simu feki kuliko kulishwa vyakula vilivyoharibika, afya ni mtaji wa kwanza
 
Hapo kuokota vyakula vilivyo expire na kuvipika kwa ajili ya wateja umereflect riwaya ya “watoto wa mama ntilie”
 
Kwa hali ya Tanzania ilivyo wala sishangai wajasiriamali wakipambana kwa udi na uvumba
 
Kuanzia matatizo ya vidonda vya tumbo, vijana kuwahi kuzeeka, kukosa nguvu za kiume, n.k. kwa kiasi kikubwa inachangiwa na kula vyakula vya mtaani kwa wapishi wasio waaminifu.

Kuna wafanyabiashara wa vyakula wao ni faida mbele, afya yako haina kipaumbele, wewe utalishwa vibovu wao watajipikia chakula tofauti.

Njia za kuweza kufaidika ni kama zifuatazo

  • Kununua nyama ya mnyama aliekufa, mgonjwa, n.k. nyama hizi ni bei rahisi zaidi
  • kwenda kuokota mizoga iliyotupwa, hasa kuku
  • kutumia mafuta ya transfoma kukaangia, yanatumika kwa muda mrefu sana.
  • kutumia mafuta yaliyo expire, ukiyaona kwenye kaangio huwa yana rangi nyeusi au brown
  • kwenda kuokota vyakula vilivyoharibika hasa mchele na kuupepeta upya
  • Kutumia nyanya, nazi na viungo vya viwandani badala ya viungo asili
  • n.k.
Usicheze na afya yako kwenye suala la chakula kuwa makini sana,ni heri ugharamike zaidi uwe unarudi kwako kula, kubeba chakula chako, kuletewa, n.k.
Katika hii Dunia ya Sasa hivi watu wanachojali ni faida tu
 
Back
Top Bottom