Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Nitasema tena na tena kuwa serikali yetu haijawahi kuwa adui kwa raia wake. Haijawahi kuwa na nia ovu kwa raia wake hata siku moja.
Watanzania wenzenu ndio wanageuka kuwa adui wa maisha yenu kisha nyie mnaisingizia serikali.
Serikali inatenga mabilioni kununua dawa kwenye Vituo vya afya, zahanani na hospitali zake lakini wahuni wanaanza kuzimezea mate . Dawa zenyewe pia zikifika kwenye bohari za MSD za kanda wahuni wanaanza kuona kama fursa imefika.
Serikali hairuhusu hakimu, karani au jaji wa mahakama kuchukua rushwa. Ubaya zaidi Watanzania wenyewe ndio tunakuwa wa kwanza kuwashawishi maafisa wa serikali kuwapa rushwa. Mnatoa rushwa wenyewe halafu mbele mnaenda kusema ile ofisi kwa rushwa hatari. Wewe mtoaji ndiye ulipaswa ufungwe first.
Serikali haijawahi kumpiga mtuhumiwa kwenye Vituo vya polisi, ni Watanzania wenzenu wanawadunda huko polisi. Serikali iko safi
Serikali inatoa pesa za barabara kila mwaka, Watanzania wenzenu ndio wanazimung'unya na kufanya miradi isikamilike kwa wakati au kuwa chini ya viwango.