Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake

Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake

eden kimario

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2015
Posts
10,356
Reaction score
16,379
Neno dogo lakini lenye marefu na mapana yake.

Hivi ni kweli kwamba unaweza ukawa na rafiki kumbe ana mipango ya Siri ya kukuangamiza kabisa! Na wewe huna hata taarifa na unaendelea kucheka nae tu?

Je, ni kweli watu wenye upendo uliopitiliza wanaweza kuwa na mipango ya Siri ya kukuangamiza kabisa! Na wewe usijue kabisa?

Je, ni kweli watu wanaosaidia Sana wengine na baadae kuacha gafla kukupa msaada bila sababu yoyote, hata ukijaribu kuuliza anakwambia nimeamua tu! Wanaweza wakawa na mipango ya Siri ya kukuangamiza bila wewe kujua chochote?

Je, ni kweli watu wa nyumbani mwako uliowazoea, na kushiriki nao Kila kitu chako wanaweza kuwa na mipango ya Siri ya kukuangamiza bila wewe kujua kabisa! Huku wakiendelea kuonyesha kuwa wanakupenda sana?

Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake hili neno Lina maanisha Nini hasa katika maisha ya kawaida Wana JF

Neno dogo lakini naona Lina ogopesha Sana hasa katika Dunia hii tunayoishi na wenzetu bila kuwajua wala kuwafahamu mipango yao juu yetu. Ina nia nzuri au mbaya.

Tusaidiane jamani
Adui wa mtu ni wa nyumbani mwake ni neno ambalo sijawahi kulielewa kabisa.
 
We ndo anza kulifaham kua ni ivyo ili ujue unaishi nao kwa taratibu zipi
 
Hili liko wazi kabisa, Mimi adui wangu wa sasa ni ndugu wa damu na alikuwa mwenye kuinesha upendo mkubwa kwangu
 
Back
Top Bottom