DR Mambo Jambo
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 11,622
- 26,005
Hivi karibuni Tarehe 19 January, 2025 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa katika Mkutano Mkuu Maalum wa Chama cha Mapinduzi CCM alisema kwamba amekuwa akipata ombi kutoka kwa Makamu wa Rais Mh. Dr. Philip Mpango la yeye kujiuzulu nafasi yake ya Umakamu na hata baadaye Dr. Mpango alimpelekea Rais Barua rasmi ya kujiuzulu.
Sasa mwananchi mmoja ambaye pia ni Wakili kwa majina ya TENZI ANTHONY NYUNDULWA alikwenda Mahakama Kuu, Masjala Kuu Dodoma akiwashtaki Dr. Philip Mpango pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwamba wamevunja sheria za nchi pamoja na Katiba Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mtu huyu alienda kuomba kibali cha mahakama ili aweze kuleta maombi ya mapitio ya kimahakama kwaajili ya Mahakama Kuu kutamka kwamba ofisi ya Makamu wa Rais ipo wazi tangu Makamu alipowasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais, Mahakama imwamuru Rais Samia kupendekeza jina la mtu mwingine ili awe Makamu wa Rais na zuio kwa Philip Mpango kusimama kama Makamu wa Rais kwakuwa nafasi yake iliondoka tangu alivyokabidhi barua yake ya kujiuzulu kwa Rais.
Mleta maombi haya Wakili Tenzi anaendelea kusema kwamba, kitendo cha Rais Samia kupokea barua ya kujiuzulu kutoka kwa Dr. Mpango na kutotamka kwamba ofisi ya Makamu wa Rais ipo wazi ni uvunjifu wa katiba na kufanya ofisi ya Makamu wa Rais kuwa chini ya mtu ambaye nafasi yake ni tata na ya mashaka.
Sasa kikawaida ili kesi kama hizi (kesi za kibali cha mapitio ya kimahakama) zikubaliwe na mtu apewe kibali na Mahakama ni lazima athibitishe baadhi ya mambo kama, kuwa na hoja katika jambo hilo, kuwa na maslahi na jambo hilo, lazima pia uambatanishe nakala ya maamuzi kama unataka ku-challenge maamuzi ya taasisi au mtu fulani, pia maombi ya kibali yafailiwe ndani ya muda (miezi sita tangu uamuzi ufanyike) na kusiwe na nafuu nyingine nje ya mapitio ya kimahakama.
Sasa katika kesi hii Mleta maombi aliuilizwa na Mahakama atoe barua ambayo Dr. Philip Mpango alimwandikia Rais Samia kujiuzulu ili mahakama iamini kama hilo swala lipo na kulitolea maamuzi kama anavyotaka., maana tofauti na hapo mahakama itakuwa inacheza kamari au kubeti swala ambalo haipo tayari kulifanya.
Mleta maombi hata hivyo alishindwa kuileta barua hiyo mahakamani na hatimaye maombi yake yakaondolewa mahakamani kwakuwa madai yake ni fununu tu ambazo ameshindwa kuthibitisha.