Adverse possesion,acquesence and law of limitation

okaoni

JF-Expert Member
Joined
Jun 25, 2011
Posts
1,471
Reaction score
1,303
Ndugu wapedwa kaka na dada wasomi.nimeandika kichwa cha habari hicho nikiomba ufafanuzi wenu wa kisheria kuhusu matamko ya wanasiasa yanayotolewa kwa watu waliojenga kwente ama hifadhi za barabara au maeneo mengine yasioruhusiwa lakini idara husika zimekuwa kimya hata baada ya kupita miaka zaidi ya 12 na daabaye wanaibukia na kuwaabia watu hao waondoke au kuwavunjia bila fidia je ni sahihi?
 
Mkuu kwenye kila wilaya au mji au jiji kuna ramani ambayo ni master plan ya jiji au mji au wilaya nzima
Master plan hiyo inaonyesha maeneo yote ikiwemo hifadhi za barabara, maeneo ya wazi, viwanja vya shule au maeneo ambayo ni proposed schools or college or hospital
Sasa kabla ya kujenga au kununua kiwanja wataalam wanashauri kwanza kufanya due diligence ya eneo husika
Ujue mipaka yake na matumizi yake na ndo maana muuzaji wa kiwanja anakuuzia "as it is" na anakuambia wazi kuwa yale aliyokuambia ndo anayoyajua na ni ya kweli
Kama kuna mengine wewe wapaswa kuchunguza
Sasa unaponunua sehem au kurithi sehem ambayo may be ni hifadhi ya barabara, wenye ardhi ambao ni serikali wanajua kuwa wewe ushafanya due diligence ukajua kuwa hili ni eneo la hifadhi ya barabara na uko pale kama mkaaji wa muda tuu na muda wowote unaweza kuondolewa watakapohitaji barabara au eneo lao
Maeneo haya hio issue ya adverse possession haiapply kwa kuwa toka mwanzo eneo sio lako na you can not claim what you dont have
So la kukushauri hapo ni kuwa makini sana unapouziwa eneo fanya uchunguzi wako binafsi kabla ya kukubali kununua eneo hilo kutoka kwenye ngazi zinazohusika maana usije ukaishia kutamani cake ambayo sio yako toka mwanzo
 
Mr.rocky ninashukuru sana kwa ushauri wako wa kitaalamu ambao nadhani hautanisaidia mimi tuu ila kwa mtu yoyote ambaye ataona kuwa una merits kwake sana sana watu wanaonunua squaters inabidi waielewe vizuri hiyo principal ya " caviet emptur"ulioifafanua kwa kina
 

Asante sana Mkuu
Nashukuru kama umefaidika na ushauri wangu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…