Afadhali tumefungwa kamoja na misri

sayoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
5,280
Reaction score
7,930
Nimeangalia gem ya Misti na Tanzania, kiukwel kiwango chetu bado sio kizuri hasa hasa kwa upande wa kiungo, namshauri kocha ikiwezekana Ajibu apande ndege haraka aende misri kidogo labda anaweza kuokoa jahazi, kwa upande wa beki naona kidogo inajitahidi, forward Sina wasi wasi nazo kabisa ila na yule dogo mbape angekuwepo ingekua poa sana , tatizo kiungo tu ndo sio kizuri
Ajibu aende haraka akaongeze nguvu, ni hayo tu maoni yangu
 
Mfumo wa Kocha ndiyo upo ivyo kupaki bus,Bocco na Farid walicheza kama wing midfielders na walikuwa wanalinda zaidi kuliko kushambulia.

Kiungo kilikuwa hakiisogezi timu mbele,leo hata pasi tatu hatujapiga zaidi ya kubutua tu.Himid Mao anajua kukaba ila huwa hajui wapi apeleke mpira (Sijawahi mkubali huyu),combination na Fei toto ilifail nilitegemea kocha amwingize Erasto Nyoni mapema sana kuongeza nguvu ila akawa anang'ata kucha tu wakati timu inashambuliwa muda wote akaingia kiungo wa Lipuli Mtoni Ally, ukizingatia hana uzoefu tukabaki vile vile tu.

Hii ni mechi ya kirafiki, wakati Kocha wa Egypt Kafanya sub kama 5hivi kocha wetu alikuwa bado anafurahia droo hadi zile dakika za 60.

Kiufupi Sisi tunamsimamizi wa mazoezi tu,nakocha anataka kupandisha cv yake kupitia Tz ndiyo maana anatutia aibu Kwa mpira wa hovyo.

Amunike akipaki bus kama leo na Senegal tutakula mkono saafi kabisa.

Tusitegemee makubwa sana

Hongera Aishi Manula kwa kubebeshwa gunia la misumari,hakika umelipambania
 
Mmeanza kuleta ujuaji wenu. Kama ni wajuzi hiyo Timu mngeshapewa nyie mfundishe. Pia mkumbuke maamuzi sio ya Amunike peke yake bali ni bench zima la ufundi. Ninauhakika huyo Ajibu angekuwepo na timu ikafungwa bado mngesema ni kwavile KICHUYA hayupo.
 
Ilo li himid sijui ni la nan na kila coach lazima ampange..... Dunia ina maajabu
 
Aina iyo ya mpira ndio iliyo mfanya Masio Maximo awe kocha aliyefanikiwa zaid kuliko kocha yoyote wa Stars hiv karibun. Miaka yote tulicheza ugenin na Mafarao tulipigwa 5 leo tumezuia na kufungwa 1. Kuna mabadiliko Chanya yanakuja taratibu.
 
Kocha alifanya makosa kumwacha bwana migomba na jonasi. Hawa ni viungo wazuri sana.

timu haiwezi kushambulia kama viugo hawana ushirikiano. Pia nadhani niwakati huyu bwana Amunike akakubali kushauriwa.

pia ni mgumu kufanya mahamuzi ya haraka kusaidia timu.
 
Emanike anafaa kuwa kocha wa viungo
 
Kwel kabisa kulikua hakuna sababu yakufanya sub moja to wakati mechi yenyewe ni ya kirafiki, ilikua afanye sub nyingi kuangalia mapungufu ya wachezaji wake na kuajua na yupo vizur zaidi
 
Yani Watanzania kila mtu ni kocha kila mtu ni mchambuzi kila mtu ni mwanamichezo yani tabu tupu

Binafsi naona uzoefu ndio tatizo na mfumo wa kocha umekuja kwasababu ya mapungufu tulio nayo ukiangalia vijana pressure ni kubwa sana kiasi kwamba wanaondoka kabisa kenye ari ya mchezo
Mmeanza kuleta ujuaji wenu. Kama ni wajuzi hiyo Timu mngeshapewa nyie mfundishe. Pia mkumbuke maamuzi sio ya Amunike peke yake bali ni bench zima la ufundi. Ninauhakika huyo Ajibu angekuwepo na timu ikafungwa bado mngesema ni kwavile KICHUYA hayupo.
 
Kama hawana nidhamu?
 
Wachezaji wetu huwa wanaishiwa maarifa wanapofanyiwa pressing kali hasa kwenye eneo la kiungo. Hata Ajibu na Mkude wangekuwepo bado tunashida kama nchi. Ni Samatta pekee na labda Erastho Nyoni ndio wanaweza kutuliza mpira na kuulinda hata wakiwa wanakabwa na watu 2 hadi 3!!

Himid anaweza kukaba vilivyo lakni hawezi kutembea na mpira hadi aupeleke sehemu salama na sahihi. Mkude anaweza kuchezesha timu lakini hana nidhamu ya ukabaji uliotimia. Fei Toto na Domayo wana kitu fulani lakini hawana 'mbavu' za kupambana na wachezaji wa kiwango cha Misri. Fei Toto ndio kwanza anaendelea kupevuka. Si rahisi kwake kushinda vita kwenye muziki wa Afcon, labda awe na back up ya viungo wawili nyuma yake kama Nyoni na Himidi Mao au hata Mkude angekuwepo.

Game ijayo hasa ya mashindano ya Algeria, natamani viungo wote, Nyoni, Fei Toto na Himid Mao wacheze kwa pamoja, Amunike aue winger moja, hasa Farid Mussa
 
Kwel kabisa kulikua hakuna sababu yakufanya sub moja to wakati mechi yenyewe ni ya kirafiki, ilikua afanye sub nyingi kuangalia mapungufu ya wachezaji wake na kuajua na yupo vizur zaidi
Muoga sana mkuu
 
Aina iyo ya mpira ndio iliyo mfanya Masio Maximo awe kocha aliyefanikiwa zaid kuliko kocha yoyote wa Stars hiv karibun. Miaka yote tulicheza ugenin na Mafarao tulipigwa 5 leo tumezuia na kufungwa 1. Kuna mabadiliko Chanya yanakuja taratibu.
Kwa mpira huo hatuwezi kufika mbali hata kwa miaka 10
 
Nimeona kitu Zimbwe Jr akicheza winga wa kushoto. .Misri ilikuwa lazima washinde mechi iliyopita walipigwa. .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…