BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Fatma Kigondo anayedaiwa kuwatuma watuhumiwa wa kosa la kubaka kwa kundi ametii wito wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dodoma iliyomtaka kufika mahakamani hapo leo Septemba 5, 2024.
Mahakama hiyo Agosti 23 ilitoa wito wa kufika mahakamani (samansi) kwa Fatma baada ya ile ya awali iliyomtaka kuhudhuria mahakamani siku hiyo kutotekelezwa.
Shauri hilo la malalamiko namba 23627 lilifunguliwa na Paulo Kisabo na kupangwa mbele ya Hakimu Mkazi Francis Kishenyi.
Licha ya Fatma kufika mahakamani hapo leo Septemba 5, shauri liliitwa mbele ya hakimu Nyamburi Tungaraja ambaye aliliahirisha hadi Oktoba 7, 2024.
Mlalamikaji Kisabo ambaye ni wakili, akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya hakimu Kishenyi kuhamishwa kituo cha kazi.
Amesema kwa sasa kesi hiyo bado haijapangiwa hakimu mwingine wa kuisikiliza.
"Huenda itakapofika Oktoba 7 mwaka huu itakuwa imeshapangiwa hakimu... Lakini leo 'afande' amefika mahakamani," amesema Kisabo.
MWANANCHI
PIA SOMA: