Afande Sele ana matatizo gani?

Kiranja Mkuu

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2010
Posts
4,219
Reaction score
4,608
Huyu jamaa sijui ana matatizo gani, kila siku ni ugomvi kwa kwenda mbele.
Aligombana na Sugu, akagombana na O Ten, akagombana tena na P Funk, amegombana na Madee, amegombana na kina Ditto waliokuwa wote kwenye kundi la Watu Pori, juzijuzi huko Morogoro kafanya fujo na kujikuta yeye na rafiki yake kipenzi 20 Percent wakitiwa ndani.
Afande Sele sasa kagombana na huyo aliyekuwa rafikiye 20%.
Tumshauri huyu mwenzetu ili ajirekebishe, ili aweze kutimiza ndoto zake za kuwa MBUNGE
 
Usichokijua nizaidi ya usiku wa kiza kinene!
 
Alianza vizuri lakini kadri siku zinavyokwenda anazidi kuporomoka,anahitaji kutulia kwa kweli, apate couselor!
 
Hajielewi elewi. Muziki umemshinda sasa anataka magazeti yaendelee kumwandika, that's why anatumia ngumi na ugomvi ili aendelee kuandikwa
 
Ndio mwimba kwaya wa dhehebu gani huyu wakuu?
 
Bange,...eti aende bangeni tena itakuaje mi sipati picha..
 
Wenye matatizo wanaogombana na selemani msindi ila jana yuko poa anasimama katika maslahi yake!big up afande bangi ni jani tu kama majani mengine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…