Afanyaje ili apate uchungu?

KAUMZA

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2010
Posts
699
Reaction score
237
Ndugu, mke wangu ni mjamzito. Makadirio ya kujifungua (due date) ilikuwa ni tarehe 10.03.2015 na kwa mujibu wa vipimo vya ultra-sound ni tarehe 13.03.2015..

Sasa muda umepita na hana dalili zozote za uchungu. Tufanye nini ili apate uchungu na hatimaye kujifungua? Maana ameanza wiki ya 41 sasa.

Nawasilisha..
 
Mungu bado ni mwema muombeeni tu na pia msimpe chochote ili kulazimisha uchungu mkazanie afanye mazoezi mtembeze mwendo mrefu I hope akifanya vivo kutakuwa na mabadiliko.Mimi nilijifungua wiki ya 41 na mwanzo ulikuwa mgumu maana nnauchungu njia haifunguki ila Maombi,mazoezi.
 
Mkuu, naomba umtoe mjamzito huyo kwa matembezi nje ! atembee kwa takariban dakika 45.. in-shaa-allah matokeo na tija itadhihiri ...hongera!
 
Mpe haki yake la tendo la ndoa; wale wazungu wakimwagika huwa wana kemikali ambayo husaidia sana kufungua njia
 
Naomba umpeleke Kwenye Kituo cha Afya au Hospitalini wana dawa watamchoma sindano ya uchungu na uchungu utamfika tu na mazoezi ya kutembea atayafanyia hukohuko.
 
hakuna tatizo atajifungua tu ndani ya hio week ya 41 or 42
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…