Afanye nini mpenzi wake amwamini?

Mjanga

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2011
Posts
1,238
Reaction score
324
jamani wana JF ni muda wa zaidi ya miaka minne sasa kuna rafiki yangu amekuwa akiishi na mchumba wake, lakini binti amwamini kabisa, mara nyingi wanakwazana, hasa jamaa akituhumiwa kuwa ni PLAYER, ilhali hayo si ya kweli! tunamsaidiaje???
nimemwakilisha coz hajajiunga ndani ya JF!
 
Kwanza karibu sana JF....
Pili,kuna sababu zinazopelekea huyo msichana kutomwamini,ni lazima amuulize hizo sababu na ajitahidi kujirekebisha ili kurudisha kuaminiwa,au pengine msichana amewahi kutendwa kwahiyo kuamini mwanaume inakuwa issue.......natamani ungeeleza zaidi,mazingira ambayo yanapelekea wao kutokuaminiana.
 
forum ya kuomba ushauri
 
Aepuke kufanya vitu au mazingira yanayoweza kumpa huyo dada wasiwasi!
 
uchumba wa zaidi ya miaka 4 ndio kikwazo.
Atangaze ndoa kama sio player na ndoa iwepo kweli!!!!!
 

1. Ajenge mazingira ya uwazi ya makusudi kabisa yatakayomfanya binie amwamini.

2. Akanushe tuhuma kuwa yeye si Player kwa vitendo mfano kushare naye information zinazotia mashaka, kumjulisha juu ya mienendo yake isiyoeleweka kama ipo.

3. Ajenge mawasiliano ya karibu naye na kuwa muwazi zaidi, kumpenda, kumjali, kumpa nafasi ya kutosha, kumheshimu nk ili kujenga trust.
 

Kama unaweza muulize huyo shemeji yako ni sababu zipi zimazomfanya asimwamini mwenzie. Ukishazifahamu hapo ndipo utaweza kutafuta namna ya kuwasaidia ili waache kukwazana na penzi lao lishamiri. Kuhusu kuwa PLAYER ana ushahidi au ni hisia tu zinazomfanya adhani hivyo? Kujua tatizo toka upande mmoja tu haitasaidia katika kutatua tatizo linalowakabili.

YouTube - Shontelle - Impossible
 
Du Mjanga kwanza karibu JF maana inaonekana umejiunga saa moja za usiku huu karibu sana
Nakushauri na mwenzako ajiunge usimsemee ili kupata ukweli kwani huenda mchumba wake ana ukweli au jamaa yako si PLAYER tunashindwa kumhukumu au kumshauri, kwani kuna magonjwa usikute ndio analolisubiri
Namshauri hivi vigozi sio deal tena km amzingua amteme apande daladala ingine
 
atumie muda mwingi akiwa na huyo mpenzi wake-hii itamuondolea huyo binti alikuwa wapi na nani/anafanya nini? 2. asifanye jambo lolote kwa kificho au kujenga mazingira yatakayopelekea mpenzi wake kuwa na wasiwasi.:coffee:
 
asimwamini huyo she,am-treat kibabe tu,ma-she cyo wa2 wa kuaminiwa.
 
:A S-alert1:
Wakuu hakuna uchumba wa miaka minne.... hata agekuwa nani lazima angehisi hivyo. Huyo dada alitegemea baada ya miezi kadhaa sasa miaka minne na anavosema player haina maana kwamba anatoka bali anamaanisha jamaa anamchezea tu!!!
 
thank you all for welcoming me to JF!and thank you all for your useful inputs on the topic! actually I find you people are helpful! ILA MSIWE TU MA-fis-ADI!:clap2::clap2::clap2::clap2:
 
atumie muda mwingi akiwa na huyo mpenzi wake-hii itamuondolea huyo binti alikuwa wapi na nani/anafanya nini? 2. asifanye jambo lolote kwa kificho au kujenga mazingira yatakayopelekea mpenzi wake kuwa na wasiwasi.:coffee:

Hata kazini aende naye au?
 
pesa sabuni ya roho.... Penye udhia penyeza rupia...
 
kuondoa udhia waongozane kama kumbikumbi tu kama wanaweza. La kila mtu ashike time yake maana uchumba wa miaka minne bila ndoa ni hasara kubwa!
as aq
 
Naona wengi wameangalia upande mmoja wa shillingi kwamba kuna vitu jamaa anafanya ambavyo vinamfanya huyu mwanamke asimuamini.Ni kweli inakuwaga hivyo vipi kama huyu mtu hana dalili hizo? Hapo ndio inakuja labda huyu mwanamke yuko insecure.


Kwahio mkuu inabidi utoe details zaidi kidogo kuhusu matukio yaliomfanya huyu dada alalamike, inawezekana makosa sio yake inaweza kuwa huyo mwanamke hajioni mzuri wa kutosha kwa rafiki yako kiasi cha kwamba anapata wasi wasi na mambo madogo madogo kwamba jamaa ana cheat.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…