AFCON: Ghana wameshinda tu kwa mbeleko ya refa

AFCON: Ghana wameshinda tu kwa mbeleko ya refa

herikipaji

JF-Expert Member
Joined
Aug 23, 2016
Posts
1,198
Reaction score
1,369
Kwa wale wanaofatilia vizuri AFCON mechi ya robo fainali ya tarehe 29 january 2017 ile ya awali kati ya Ghana na Congo refa B. Camille wa huu mchezo amewapa penati "NYEPESI" Ghana na kufanya washinde kwa mbeleko ya huyo refa.

Ukiangalia kwa umakini utangundua yule mshambuliaji Atsu alijiangusha kwa makusudi tu wapate penati na kweli refa naye kawazawadia penati ambayo hata hawakustahili na kupata goli la pili.

Mchezo ulikuwa mzuri sana kutazama lakini hatimaye refa kauharibu kwa maamuzi ya kutoa penati isiyo kuwa na maana na kusababisha Congo kuaga mashindano.
 
Kongo ilikuwa inauwezo wa kuchukua kombe hili
 
Mbeleko noma sana Jana Congo walipiga mpira mwingi sana maana kipindi cha kwanza walikosa magoli mengi sana
 
ghana hata mechi na uganda.. walipewa penati nyepesi sana...

africa ndio maana hatufanyi vizuri world cup.. tunapenda sana kubebana bebanaaaa...
 
ghana hata mechi na uganda.. walipewa penati nyepesi sana...

africa ndio maana hatufanyi vizuri world cup.. tunapenda sana kubebana bebanaaaa...
Mkuu Afrika matatizo yani ni kila kona sasa hata kwenye michezo magumashi kibao.
Siku ile tena Ghana walizidiwa sana na the cranes, halafu mchezo unakuwa mzuri refa anatoa penati ya kipuuzi ili tu kuwabeba mimi naona sasa hata kundelea kutazama hii michuano siwezi maana imejaa ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom