Timu ya Taifa ya Senegal imefanikiwa kuingia Hatua ya 16 Bora ya Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), leo Januari 19, 2024 kwa kuifunga Cameroon magoli 3-1, hivyo kufikisha pointi 6 katika Kundi C ikiwa imesaliwa na mchezo mmoja.
Magoli ya Senegal yamewekwa wavuni na Ismaila Sarr, Habib Diallo na Sadio Mane wakati lile la Cameroon likifungwa na Jean-Charles Castelletto.
Michezo ya mwisho Hatua ya Makundi kwa timu hizo, Senegal itacheza na Guinea huku Cameroon yenye pointi moja ikitarajiwa kucheza dhidi ya Gambia.