Afghanistan: Shambulio baya lakumba msikiti wa Kunduz wakati wa ibada ya Ijumaa

Afghanistan: Shambulio baya lakumba msikiti wa Kunduz wakati wa ibada ya Ijumaa

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2018
Posts
21,711
Reaction score
35,644
Mlipuaji wa kujitolea muhanga amelenga msikiti mmoja kaskazini mwa mji wa Afghanistan wa Kunduz wakati wa ibada ya Ijumaa na kuwaua takriban watu 50.

Picha katika mitandao ya Kijamii zimeonesha miili na vifusi ndani ya msikiti , unaotumika sana na jamii ya walio wachache wa dhehebu la Shia.

Hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulio hilo.

Waislamu wenye itikadi kali wa dhehebu la Sunni ikiwemo kundi la wapiganaji wa Islamic State, wamelenga jamii ya Washia kwasababu wanawachukulia kuwa watu wazushi.

Tawi la IS-K la kundi la IS nchini Afghan ambalo linapinga kundi la wapiganaji wa Taliban, limetekeleza mashambulizi kadhaa ya mabomu hivi majuzi likilenga eneo la mashariki mwa taifa hilo.

Mfanyabiashara wa eneo hilo Zalmai Alokzai, ambaye alikimbia hadi katika hospitali kutazama iwapo madaktari walihitaji damu, alielezea kuona picha za kutisha.

''Ambyulansi zilikuwa zikienda na kurudi katika eneo la shambulio hilo kubeba miili', aliambia chombo cha habari cha AFP

Huku kukiwa hakuna ambaye ametangaza kuhusika na shambulio hilo kufikia sasa, shambulio hilo lina dalili za ;kutekelezwa na IS-K , kundi lililoshambulia uwanja wa ndege wa Kabul mwezi Agosti.

Kundi hilo liliwalenga jamii ya wachache wa dhehebu la Shia hapo awali, huku wauaji wa kujitolea muhanga wakishambulia misikiti , klabu za michezo na shule.

Katika wiki za hivi karibuni, kundi la wapiganaji wa IS limeanzisha kampeni ya mashambulizi dhidi ya wapiganaji wa kundi la Taliban.

Kundi la IS lilishambulia ibada ya wafu iliohudhuriwa na idadi kubwa ya viongozi wakuu wa Taliban mjini Kabul siku ya Jumapili, na kumekuwa na msururu wa mashambulizi madogo katika mkoa wa mashariki wa Nangarhar na kunar, ambapo IS ilikuwa na ngome yake.

Mashambulizi ya Ijumaa iwapo yalitekelezwa na kundi la wapiganaji wa IS , yataidhinisha upanuzi wa vitendo vyake katika eneo la kaskazini la taifa hilo.

Taliban inasema kwamba imewakamata makumi ya wanachama wa kundi la IS na wanaaminika kuwaua wengine wanaoshukiwa kuwa na uhusiano na kundi hilo, lakini pia wamepuuza tisho la IS.

Raia wengi wa Afghanistan walitumai kwamba ujio wa utawala wa Taliban nchini Afghanistan ungeleta amani badala ya uongozi wa kiimla.

Lakini IS inawakilisha tishio kubwa kwa ahadi zake za kuimarisha usalama.

Taliban ilichukuwa udhibiti wa Afghanistan baada ya wanajeshi wa kigeni kuondoka nchini humo mwezi Agosti kufuatia makubaliano kati ya Marekani na Taliban , miongo miwili baada vikosi vya Marekani kuwaondoa wapiganaji hao katika mamlaka 2001.

Screenshot_20211008-183200_Facebook.jpg
 
Duuuh HAVOC.....

Nashukuru kuwa mtanzania....

Najivunia kuwa mtanzania......


Eeeeh taifa letu "teule kiamani"[emoji120]

#SiempreJMT
#TanzaniaKwanzaKablaYaNafsiZetu
[emoji120][emoji2532][emoji120][emoji2532]
 
Acha ujinga wako wewe!!! Husikii Watanzania wanaolia kuhusu watu wao kupotea kwa miaka sasa na Serikali iko kimya na wala hakuna uchunguzi? Husikiii watu kukamatwa kwa kufanya jogging tu au kuikosoa Serikali? Husikii watu kuporwa billions of their money na TRA au TAKUKURU kwa uongo uongo tu? Husikii watu kubambikiwa kesi FEKI na kuwekwa lupango miaka chungu nzima kisha kuachiwa bila fidia eti Serikali haitaki tena kuendelea na mashtaka? Acha kuonyesha ujuha wako hadharani. Tanzania hakuna AMANI hakuna HAKI.

Kama huko Tanzania hata kusikia tu hutusikii uliko?!!!

AMANI NA UTULIVU
AMANI NA UTULIVU
AMANI NA UTULIVU

UPENDO NA UMOJA
UPENDO NA UMOJA
UPENDO NA UMOJA

Hayo ni madogo kwako?!!!
 
Kama ingewezekana, ungejaribu kwenda kuishi kule Afghanistan; hapa nadhani ungeona tofauti na kutambua kwanini tunajivunia amani.
😍😍
Huko kumewashinda Askari wa Marekani waliopigana miaka 20...mwishowe wakaamua kutema ndoano na kuwaachia nchi "maswahiba zao Taliban".....

Anajiongelesha tu mkuu wangu.....

#TANZANIA YA AMANI NA UTULIVU
 
Kama huko Tanzania hata kusikia tu hutusikii uliko?!!!

AMANI NA UTULIVU
AMANI NA UTULIVU
AMANI NA UTULIVU

UPENDO NA UMOJA
UPENDO NA UMOJA
UPENDO NA UMOJA

Hayo ni madogo kwako?!!!
Nchi nyingi duniani zina hivyo vitu pia, kuna vitu vya maana kama kuboresha maisha ya watu kwa kufungua masoko ya bidhaa zinazozalishwa, kupunguza ukosefu wa ajira na umaskini, kukua kidemokrasia na haki za binadamu. Amani na Utulivu hazileti mkate mezani na shida zinavyozidi hivyo ulivyovitaja vyote vitatoweka.
 
Nchi nyingi duniani zina hivyo vitu pia, kuna vitu vya maana kama kuboresha maisha ya watu kwa kufungua masoko ya bidhaa zinazozalishwa, kupunguza ukosefu wa ajira na umaskini, kukua kidemokrasia na haki za binadamu. Amani na Utulivu hazileti mkate mezani na shida zinavyozidi hivyo ulivyovitaja vyote vitatoweka.
Sasa uwe na hivyo vyote ulivyoorodhesha halafu uone pale unapokosa AMANI NA UTULIVU....
 
Back
Top Bottom