Afikishwa Mahakamani kwa kutoa risiti feki za mauzo ya bilioni 1.8

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Serikali imemfikisha katika mahakama ya hakimu mkazi Arusha Afisa mauzo kutoka kampuni ya royal colour paint limited anayejulikana kwa jina la Silvester Charles akikabiliwa na makosa matatu utakatishaji fedha, kutoa risiti zisizo halali za malipo pamoja na kuisababishia mamlaka ya mapato Tanzania TRA hasara ya zaidi ya bilioni moja nukta nane.

Shauri hilo la uhujumi uchumi namba 4593/ 2025 limefikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza na mamlaka ya mapato Tanzania TRA.

Soma Pia: Dar: Mafundi wa EFD wafikishwa Mahakamani kwa kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Milioni 954.5


Wakili wa Jamhuri Godfrey Nugu amesema miongoni mwa makosa hayo kotoa risiti zisizo halali au risiti feki za zaidi ya shillingi bilioni moja na milioni mia nane ambapo mshtakiwa huyo alitoa risiti hizo akionesha kuwa kampuni ya royal paint center limited imefanya mauzo ya kiasi hicho .

Your browser is not able to display this video.
 
Huyu jamaa anaakili sana, watanzania tumpongeze.

Watawala wanalipana pesa kama hizi kila siku, halafu hakuna wanachokifanya, halafu huyu kajiongeza mnampeleka mahakamani.
 
Kwa hiyo Sylvester anajifanya mwana CCM kuiba hela bila kufikiri?
 
Daaa basi sawaa....acha wapambane na watawala...
 
Ila wao wakiiba hawakamatani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…