DOKEZO Afisa Elimu kata ya Kasekese anatumia madaraka yake vibaya, Serikali tunaomba mtuondolee

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

GUY LUEMBA

New Member
Joined
May 19, 2024
Posts
1
Reaction score
2
Rais Samia salaam!

Ni furaha kuona umekuja kutembelea mkoa wetu wa Katavi. Furaha imetuelemea tuliposikia kwamba safari yako ni ya kichama zaidi na sio kiserikali ingawa ni vigumu kutofautisha ukiwa na safari ya kichama na Kiserikali kwakuwa mapokezi na mambo ya itifaki ni yaleyale.

Tuachane na hilo, Mwenyekiti tunaomba uje Karema kuona mradi wa bandari na barabara lakini uone umuhimu wa kuharakisha reli kutoka Mpanda Mjini hadi Karema. Pia simama kijiji cha Kasekese wananchi tuna kilio chetu kikubwa juu ya Afisa elimu kata anaitwa Luca Mwanchali.

Tangu amekuja Kasekese kutoka kusikojulikana ufaulu wa shule za kata ya Kasekese umeshuka kwa zaidi ya asiliimia 50. Shule yetu kongwe ya msingi Kasekese sasa hata nafasi ya 50 kimkoa haipo kutoka nafadi ya 1 kabla ya kuja kwake mwaka 2021. Shida ipo tena kubwa ngoja tukufahamishe.

Kijana huyu jeuri mwenye maneno ya karaha na kuudhi anapowasiliana na walimu amezua migogoro katika kila shule iliyopo kata hii huku akiwatishia kuwafukuzisha kazi, matusi mbele ya wanafunzi kutukana walimu wetu na kuwachongea walimu wakuu na kuwahamisha iwapo mwalimu huyo hataki kutoa fedha za kuendeshea shule( capitation grant ya elimu bure) kwa matumizi binafsi.

Mwezi wa nne kijiji cha Kasekese tulifanya mkutano mkuu na moja ya azimio tulimkataa Mwanchali apelekwe kata nyingine ili turudishe amani ya Walimu wetu ambao wamekata tamaa ya kazi.

Muhtasari umepelekwa kwa mkurugenzi mtendaji wilaya na yuko kimya.

Afisa elimu sekondari amekuja na kufanya vikao na Walimu wakamueleza shida zilizopo mbele ya Mwanchali lakin hakuna hatua.

Walimu wetu wanaitwa Halmashauri kupigwa mikwara na kurudi na kulazimishwa wampe fedha anazotaka bila kuwa na uhalali nazo.

Mwenyekiti, mbaya zaidi amemnunua mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Tanganyika Kibiriti na kuja kufanya mkutano wa hadhara na kuishia kututishia sana na kwamba Mwanchali anakataliwa na wana CHADEMA hivyo walimu wetu wote wanachama wa CHADEMA. Mbaya zaidi tumeambiwa kama tunataka ahame tukae vikao tuandike muhtasari tupeleke CCM wilaya ili ajadiliwe ndo CCM ipendekeze hatua za kumchukulia. Ndio utaratibu wa utumishi huu?

Mwenyekiti, tukutonye jambo, barua ya Mwanchali inasoma Afsa Elimu Kata ya Mishamo sio Kasekese. Alifanikiwa kwenda Kasekese kwa rushwa kwa kumuuzia nyumba afisa elimu msingi kwa bei ya milioni 6 nyumba ambayo alikuwa anauza milioni 15 kwa lengo la kuachwa aende Kasekese. Ndio maana afisa elimu hana kauli kwake zaidi ya kuwakaripia walimu.

Hatupendi kuchukua sheria mkononi ndio maana baada ya kusikia unakuja tukasema tukusubiri ufike na usimame kasekese ili tukueleze mengi tuliyonayo.

Tunaomba utume TAKUKURU waje kukagua wakupe mjeresho wa ubadhirifu wa Mwanchali kwenye fedha za elimu bure.

Hatuna nia ya kuhamia upinzani ila tukuombe ufanye mabadiriko ya haraka atoke mratibu huyu kwani tupo tayari kuchagua upinzani kwa hamasa kubwa ili kuanza kupingana na CCM ambao wanatutisha kwa njaa zao wanaochukua fedha kwa mwanchali.

Kiufupi mwanchali hafai kuwa afisa elimu kata popote pale nchi hii.anachoweza ni kugomanisha walimu ili awatawale.

TUNAKUAMINI MWENYEKITI WETU WA CHAMA TAIFA
MOMRADE DKT. SAMIA S. HASSAN
 
Wewe mwalimu acha hizo. Afisa elimu kata kama ana shida ungewasiosha kwa afisa elimu wilaya tu. Kuliko kumsagia kunguni huku na ukijua fika hana sehem ya kujitetea humu.
 
ccm hoyeee alisikika muriro
GSY2ZwAWwAAXivk.jpg
 
yaani afisa elimu KATA anafanya hayo yote mumekaa mko kimya....eti mpaka rais aingilie? Acheni ujinga sasa
 
Afisa elimu kata tu unamuanzishia Uzi? Huyo Hana la kukufanya mwalimu....... Mkateni mabanzi tu. Wilaya ya Tanganyika ndio Poli kuliko zote nadhani duniani.
 
AEK ndio wa kukufanya umuite rais asolve. Nyie walimu wa Tanganyika kwahyo hata hierarchy ya idara yenu ya elimu hamuijui???? Kama una evidence si upande kwa RAS kama hausikilizwi ngazi ya wilaya.
 
Pole sana man!!

Wenye mhimili was hili taifa naomba mbadili mtazamo kuhusu chadema coz chadema no chama kama vingine na tena chadema nimtoto was CCM!!

Kumekua na ombwe katika Taifa hili kwamba mtz kuwa mwanachadema no hatari zaidi ya kirusi Cha ukimwi!!!

Ukiitwa chadema mtaani umekwisha hasta hao wanaoitwa potea potea utakuta wanahusishwa na chadema!!
 
Qeww
Rais Samia salaam!

Ni furaha kuona umekuja kutembelea mkoa wetu wa Katavi. Furaha imetuelemea tuliposikia kwamba safari yako ni ya kichama zaidi na sio kiserikali ingawa ni vigumu kutofautisha ukiwa na safari ya kichama na Kiserikali kwakuwa mapokezi na mambo ya itifaki ni yaleyale.

Tuachane na hilo, Mwenyekiti tunaomba uje Karema kuona mradi wa bandari na barabara lakini uone umuhimu wa kuharakisha reli kutoka Mpanda Mjini hadi Karema. Pia simama kijiji cha Kasekese wananchi tuna kilio chetu kikubwa juu ya Afisa elimu kata anaitwa Luca Mwanchali.

Tangu amekuja Kasekese kutoka kusikojulikana ufaulu wa shule za kata ya Kasekese umeshuka kwa zaidi ya asiliimia 50. Shule yetu kongwe ya msingi Kasekese sasa hata nafasi ya 50 kimkoa haipo kutoka nafadi ya 1 kabla ya kuja kwake mwaka 2021. Shida ipo tena kubwa ngoja tukufahamishe.

Kijana huyu jeuri mwenye maneno ya karaha na kuudhi anapowasiliana na walimu amezua migogoro katika kila shule iliyopo kata hii huku akiwatishia kuwafukuzisha kazi, matusi mbele ya wanafunzi kutukana walimu wetu na kuwachongea walimu wakuu na kuwahamisha iwapo mwalimu huyo hataki kutoa fedha za kuendeshea shule( capitation grant ya elimu bure) kwa matumizi binafsi.

Mwezi wa nne kijiji cha Kasekese tulifanya mkutano mkuu na moja ya azimio tulimkataa Mwanchali apelekwe kata nyingine ili turudishe amani ya Walimu wetu ambao wamekata tamaa ya kazi.

Muhtasari umepelekwa kwa mkurugenzi mtendaji wilaya na yuko kimya.

Afisa elimu sekondari amekuja na kufanya vikao na Walimu wakamueleza shida zilizopo mbele ya Mwanchali lakin hakuna hatua.

Walimu wetu wanaitwa Halmashauri kupigwa mikwara na kurudi na kulazimishwa wampe fedha anazotaka bila kuwa na uhalali nazo.

Mwenyekiti, mbaya zaidi amemnunua mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Tanganyika Kibiriti na kuja kufanya mkutano wa hadhara na kuishia kututishia sana na kwamba Mwanchali anakataliwa na wana CHADEMA hivyo walimu wetu wote wanachama wa CHADEMA. Mbaya zaidi tumeambiwa kama tunataka ahame tukae vikao tuandike muhtasari tupeleke CCM wilaya ili ajadiliwe ndo CCM ipendekeze hatua za kumchukulia. Ndio utaratibu wa utumishi huu?

Mwenyekiti, tukutonye jambo, barua ya Mwanchali inasoma Afsa Elimu Kata ya Mishamo sio Kasekese. Alifanikiwa kwenda Kasekese kwa rushwa kwa kumuuzia nyumba afisa elimu msingi kwa bei ya milioni 6 nyumba ambayo alikuwa anauza milioni 15 kwa lengo la kuachwa aende Kasekese. Ndio maana afisa elimu hana kauli kwake zaidi ya kuwakaripia walimu.

Hatupendi kuchukua sheria mkononi ndio maana baada ya kusikia unakuja tukasema tukusubiri ufike na usimame kasekese ili tukueleze mengi tuliyonayo.

Tunaomba utume TAKUKURU waje kukagua wakupe mjeresho wa ubadhirifu wa Mwanchali kwenye fedha za elimu bure.

Hatuna nia ya kuhamia upinzani ila tukuombe ufanye mabadiriko ya haraka atoke mratibu huyu kwani tupo tayari kuchagua upinzani kwa hamasa kubwa ili kuanza kupingana na CCM ambao wanatutisha kwa njaa zao wanaochukua fedha kwa mwanchali.

Kiufupi mwanchali hafai kuwa afisa elimu kata popote pale nchi hii.anachoweza ni kugomanisha walimu ili awatawale.

TUNAKUAMINI MWENYEKITI WETU WA CHAMA TAIFA
MOMRADE DKT. SAMIA S.
Wewe ni MWALIMU
.....
 
Back
Top Bottom