Afisa Mtendaji wa Endashang'weti - Karatu aanguka na kuteguka mguu akiwakimbia wagombea wa CHADEMA

mumburya

JF-Expert Member
Joined
Mar 19, 2012
Posts
321
Reaction score
448
Dunia haiishi vituko, safari hii ni huyu Afisa Mtendaji wa kijiji cha Endashang'weti kilichopo Wilayani ya Karatu anayefahamika kama Raymond Mwasha.

Akiwa hajui hili wala lile alifika Ofisini saa 3 hivi na kukuta pasipo kutarajia wagombea wa ujumbe wa Serikali ya kijiji na mgombea uenyekiti wakiwa wanamsubiri toka jana.

Jamaa badala ya kufungua ofisi alianza kutimua mbio, bahati mbaya alianguka na kuteguka mguu. Hivi sasa anapatiwa matibabu katika hopsitali ya wilaya. Yeye anadai aliona kundi la majini akaogopa. Tutasikia mengi awamu hii. Picha zinafuata.

Maendeleo haya na vyama.
 
Hiyo kesi watabebeshwa wagombea wa CHADEMA kuanguka na kuteguka mguu hakutaonekana,kitakachosemwa ni tofauti na hali halisi ya kile kilichotokea, kuna hatari wagombea wote waliokuwepo wataushuhudia uchaguzi kwa kuchungulia kwenye matundu ya jela.
 
Labda kwa sababu hawako serikalini
 
Hapo wagombea Wa chadema wajiandae kubambikwa kesi ya nguvu.
 
Kama ni kweli, alistahili kukatika mguu na wala siyo kuteguka. Viongozi na watendaji wendawazimu, ni maadui wa Taifa letu.
 
Hahah tupunguze stresa mkuu.
hahahha, ni kweli. Ndio maana mwenzio nishaweka JF ndio kipau mbele changu, bora nikatiwe maji nyumbani kwangu au nilale giza kwa kukosa hela ya luku lakini niwe na bando la kuingia JF. tehe tehe tehe
 
SI angevunjika kiuno aisee 📴
 
Nikulipe mshahara na nikupe gari halafu umtangaze mshindi mwingine (in jiwe's voice)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…