Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 4,876
- 1,549
Job tittle: Afisa uzalishaji
Majukumu ya kazi
Masharti ya jumla kwa nafasi ya kazi
Mwenyekiti wa BBodi
Chawakim Cooperative Soceity
S.L.P 30871,
KIBAHA TANZANIA
E mail: chawakim@yahoo.com
Mwisho wa kutuma maombi: 10th February 2020
Majukumu ya kazi
- Kusimamia shughuli zote za idara ya Uzalishaji wa bidhaa za maziwa.
- Kuhakikisha kuwa anapokea maziwa yenye ubora kutoka kwa wafugaji.
- Kuhakikisha kuwa bidhaa anayoizalisha inakuwa na ubora kulingana na viwango vya TBS
- Kuandaa mpango wa uzalishaji kulingana na mahitaji ya soko
- Kuhakikisha rasilimali na malighafi zinatumika ipasavyo kwa kuzingatia Good Manufacturing Practice (GMP) na Good Hygienic Practice (GHP
- Kutimiza majukumu mengine atakayopangiwa na Mkuu wake wa kazi
- Kuweka kumbukumbu za uzalishaji siku hadi siku
- Kutoa ushauri wa kitaalamu kwa wafugaji ili kuweza kupata maziwa yenye ubora.
- Awe na umri wa miaka 25 na kuendelea
- Awe na Shahada ya Sayansi ya Chakula na Teknologia (Bachelor of Science in Food Science and Technology) au Shahada ya Sayansi ya Lishe ya Binadamu (Bachelor of Science in Human Nutrition) kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA
- Awe na uzoefu katika nafasi aliyoomba.
- Awe na ujuzi wa kutumia computer
- Awe mbunifu (creative) na mwenye bidii katika kazi bila kusimamiwa.
- Awe hajawahi kupatikana na kosa la jina.
Masharti ya jumla kwa nafasi ya kazi
- Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania
- Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa
- Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika, Barua iliyoandikwa kwa mkono na kusainia.
- Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, maelezo, nakala za vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika, Vyeti vya kitaaluma (Professional Certificate from respective Board)
- Testmonials” “Provisional Results”, “Statement of results” hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA
- Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NECTA, na NACTE)
- Mwombaji atakayeitwa kwenye usaili aje na vyeti halisi siku ya usaili
- Mwombaji atajigharamia mwenyewe wakati wa usail
- Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kughushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
- Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA
- Maombi yote yatumwe kupitia anuani tajwa hapa chini.
Mwenyekiti wa BBodi
Chawakim Cooperative Soceity
S.L.P 30871,
KIBAHA TANZANIA
E mail: chawakim@yahoo.com
Mwisho wa kutuma maombi: 10th February 2020