Rula ya Mafisadi
JF-Expert Member
- Dec 28, 2024
- 404
- 852
Anaandika Remigius Celestine Mjumbe wa Secretarieti CHADEMA Makao Makuu.
===
Mjumbe Baraza Kuu, Mkutano Mkuu na wanachama wote nawasalimu kwa salaamu ya Chama.
Bila kukupotezea Muda naomba kukushirikisha kauli nzito na muhimu kwa wakati huu iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Chama Taifa.
Ilikuwa ni mwaka 2022 mimi Remigius nikiwa na viongozi wengine wa Chama watatu kwa najina yao, Lyenda, Apollo, pamoja na Katibu Mkuu tulikuwa tunatoka Morogoro kwenye Shughuli za Chama wote tukiwa kwenye gari moja la Katibu Mkuu na Dereva akiwa Mzee Leonard Ntukula
Katibu Mkuu akaanza kutueleza mambo kadhaa akitutaka vijana tukilinde Chama.
Tukamuuliza KM kulikoni? Akasema " Chadema Tunajifurahisha lakini hatuwezi kushika dola chini ya utawala wa Mwenyekiti Mbowe "
Tulishtuka sana na tukataka kujua zaidi, tukamuuliza kwanini unasema hivyo?
Ndipo KM akafunguka, akasema Mwenyekiti Mbowe amefanya Chadema iondoke kwenye misingi yake tangu alipomleta Lowasa ndani ya Chadema.
Akaendelea kusema kwasasa Chadema hatuna meno na wala kamwe hatuwezi kushika dola. Akaendelea kusisitiza kuwa hata ile slogan ya Chadema ya Mabadiliko Lowassa , Lowassa Mabadiliko ilikuwa ni slogan tu ya Kishetani yenye Chukizo mbele za Mungu. (Kumbuka KM ni Mkatoliki mzuri pengine hili jambo aliliona kiroho)
Akaendelea kusema kuwa huwezi kuzungusha mikono kwa kwenda mbele wakati huo unazungusha mikono kwa kurudi nyuma. Akasema kwa mtu wa kawaida huwezi kuliona hili jambo. Tafsri ya hii slogan ni kuwa tunapiga hatua kwa kwenda mbele na wakati huo huo tunapiga hatua kwa kurudi nyuma.
Tukamuuliza na Wewe ulikuwepo kama Naibu Katibu Mkuu, akasema Yeye ni Mweupe na hakushiriki uchafu huo, aulizwe Mwenyekiti atawajibu. (Ukweli ni kwamba Mhe. Mnyika alisusa hakukubalia kabisa ujio wa Lowassa kwenye hili alimtetea sana Dr. Slaa)
Tukamuuliza tunatokaje hapa? KM, akasema ni mambo mawili;
a) Mwenyikiti Mbowe atoke hadharani atubu na kuomba radhi wanachadema na watanzania kwa ujumla Mungu atatusamehe tutaweza kurudi kwenye Mstari.
b) Vijana Chukueni Hatua ya kukilinda Chama.
Ndugu wapiga kura haya hayakuwa mazungumzo ya siri, hakuna siri kwenye watu 5. Na wala Katibu Mkuu hakutaka kazi ifanyike sirini alitaka muda ukifika iwe hadharani kwa kila mtu ajue.
Ikumbukwe Katibu Mkuu ni Msaidizi na Mteule wa Mwenyekiti ni mtu wa karibu sana hivyo alitaka tufanye kitu alishajua kuna sehemu kwenye Chama Panavuja. Anayajua mengi kuliko sisi wengine. Kuhakikisha hili jambo linafanikiwa tulipeana Majina ya kazi Katibu Mkuu Mnyika alinipa mimi Remigius jina la RPG (wengi wanalijua hili jina ila hawajui lilitoka wapi ) Na Lyeda alimpa jina Katibu Mkuu kuwa atakuwa anaitwa Prof. JJ kwa udhubutu wake wa kutaka tukilinde Chama.
Ndugu wanachama na wapiga kura, kwa bahati mbaya sana KM na Secretariat yake yote wanamuunga Mkono Mwenyekiti, sisi tuliopewa jukumu na Katibu Mkuu tunajiuliza Je amesahau ? Au anafanya Kusudi? Kama kasahau mimi ninaomba kumkumbusha na naomba pia asimamie kile anachokiamini kuhusu Mwenyekiti Mbowe.
Kwa kuwa hadi muda huu Mwenyekiti Hajawai kutoka na kuomba radhi. Hivyo hatua inayofuata ni ile aliyotushauli Katibu Mkuu "kukilinda Chama" kwa kumchagua Tundu Lissu.
Ndugu Mjumbe na Mpiga kura, kwa hatua hii tunahitaji watu wa kusimama na kuhesabiwa. Tunahitaji tumueleze Katibu Mkuu ukweli na yeye atoke aseme ukweli anaoujua dhidi ya Mwenyekiti ili Chama hiki tukilinde kwa wivu mkubwa. Katibu Mkuu asijifiche.
Hakikisha ujumbe huu unamfikia Mhe. Katibu Mkuu, tunahitaji atoke asituache njiani, alitupa kazi , asitukimbie na kuwa upande ule ule aliosema kamwe hatuwezi kuchukua Dola.