Afisa wa polisi ashtakiwa kwa kupoteza bunduki,akana shtaka.

Afisa wa polisi ashtakiwa kwa kupoteza bunduki,akana shtaka.

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Posts
23,718
Reaction score
66,267
Afisa mmoja wa polisi kenya katika kikosi cha Recce, mapema ijumaa alifikishwa mbele ya mahakama ya Nyeri na kushtakiwa kwa kosa la kupoteza bunduki yake.

Bwana Mike Mutwiri Mbuba alishtakiwa kuwa mnamo usiku wa julai 13-14 2016 akiwa katika kambi ya mafunzo ya polisi wa Recce ilivyo Solio Ranch eneobunge la Kieni, Kaunti ya Nyeri, kinyume na sheria aliacha bunduki yake chini ya godoro jambo ambalo lilisababisha bunduki hiyo kupotea.

Bwana Mutwiri hata hivyo alikana makosa hayo mbele ya Hakimu mkazi Onesmus Towet.

Aliachiwa kwa dhamana ya sh50000 au pesa taslimu sh40000. Upande wa mashtaka ulisema wapo na polisi saba watakaotoa ushahidi kuhusiana na kisa hicho siku ya kusikilizwa tena mnamo julai 21,2016.

Chanzo - Taifa leo.
 
Back
Top Bottom