Afisaelimu sekondari wilaya ya itilima mkoani simiyu awavua madaraka wakuu wa shule kinyemela

Afisaelimu sekondari wilaya ya itilima mkoani simiyu awavua madaraka wakuu wa shule kinyemela

Joined
Nov 26, 2013
Posts
22
Reaction score
2
Katika hali isiyo ya kawaida na iliyowashangaza watu wengi wakazi wa wilaya mpya ya Itilima mkoani Simiyu Afisaelimu huyo amewapa uhamisho wakuu wa shule zaidi ya 10 na kuwavua madaraka wengine wapatao 3 bila hata kutoa sababu za kufanya hivyo.
Watu wanajiuliza swali;je, Halmashauri hii inazopesa za kuwalipa walimu hawa kabla hawajahamia vituo vyao vipya vya kazi?
Lakini cha kushangaza zaidi ni kwamba barua hizo hazina nakala mahali popote mbali na kwa mratibu elimu wa kata ambako mkuu husika anahamia. Hii maana yake ni kuwa huenda watu muhimu kama Mkurugenzi wa Halmashauri ya Itilima, REO wa mkoa wa Simiyu,Mkaguzi Mkuu wa shule wa kanda ya Magharibi hawana taarifa na mabadiliko haya.
Je,hii si kusema kuwa barua hizi zimetolewa kinyemela?
Ni vema wahusika wafanye uchunguzi wa kina juu ya uonevu huu kwa walimu na hatua stahiki zichukuliwe kabla DEO huyu hajaleta madhara makubwa katika upande wa elimu kwani walimu hawa hawana tena ari ya kufanya kazi kikamilifu
 
Beurocracy................!

Nnavyo jua ukihamishwa lazima kuwe na documented reason and information to all required.
Pia kama ni mimi siwezi kuhama/ kuhamia kwenye kituo kipya kama sija pewa fungu la uhamisho.
 
Back
Top Bottom