Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Mada maalum ya uzao wa Afrika ambao haufahamiki sehemu kubwa ya dunia.. Ni picha na habari kwa niaba ya FB na mitandao mingine
SIRI ILIYOFICHUKA KUHUSU MILLI VANILLI.
MILLI VANILLI ni kikundi cha watu wawili ambao ni FAB MORVAN na ROBERT PILATUS, watu ambao walitumika kama wanamuziki kutokea Ujerumani.
Kundi hili liliundwa mwaka 1988 na FRANK FARIAN ambaye alitumika kama meneja wao machoni mwa watu.
Kundi hili lilitamba na kibao kimoja wapo kilichotamba kimataifa kilichoitwa GIRL YOU KNOW IT'S TRUE, kibao kilichoitambulisha albam yao iliyoitwa ALL OR NOTHING, albam uliyofanya vizuri na kufanya mauzo ya nakala mamilion kupelekea kuchukua tuzo za Grammy mwaka 1990 katika kipengele cha wasanii wapya waliochipukia.
KILICHOWAPATA
Kutokana na umaarufu walioupata na kutajirika ndipo ule msemo usemao MASIKINI AKIPATA, ........ULIA MBWATA ulidhihirika.
Taarifa ilianza kuvuja kuhusiana na kundi hili kufanya udanganyifu katika kazi yao ya muziki.
Na chanzo cha uvujishaji wa habari hizo za siri ni mmoja wa member wa kundi hilo kuivujisha ambaye alikuwa ni ROBERT PILATUS.
Siri iliyovuja ni kwamba sauti zote zilizotumika katika albam yao iliyobeba nyimbo zao zote zilizouza na kuwapa umaarufu Duniani kote hazikuwa sauti zao.
Hiyo ilipelekea KUNYAN'GANYWA TUZO ZAO.
Kabla ya kunyan'ganywa tuzo hizo waliandaliwa live acapela show jukwaani kuimba nyimbo zao ambapo walishindwa kabisa kutokana na kutojua kabisa lugha ya Kiingereza.
Baada ya hapo kundi lililega lega baada ya meneja wao kutokomea zake, hii ikapelekea ROBERT PILATUS kujiingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya.
Ilipofika mwaka 1998 walijipanga kurudi upya kwa kuandaa albam iliyoitwa BACK AND IN ATTACK albam ambayo haikufanikiwa kutoka baada ya kifo cha ROBERT PILATUS ambaye alikutwa amejifia kwa maelezo ya kwamba alitumia madawa kupitiliza, hiyo albam ilibidi kufutwa kabisa.
Pia inasemekana ROBERT PILATUS alichanganyiwa sumu kwenye madawa na huyo meneja ambaye aliwatumia wauzaji wamuangamize maana aliendelea kuvujisha mengi kuhusiana na wao.
REST IN PEACE ROB PILATUS, WE GONNA MISS YOU.
Written by Makacha