africa unite

africa unite

shokolokobangosha

New Member
Joined
Aug 24, 2013
Posts
1
Reaction score
0
ni kwa mara ya kwanza, tafadhali naomba nisemee hili, simaanishi mara ya kwanza kuzungumziwa, la hasha, namaanisha mara ya kwanza mimi kulizungumzia, ni kuhusu nmuungano wa nchi za afrika na kuwa nch mmoja, nimewaza kwa kina kwanini wenzetu wa magharibi wamelitekeleza hili mapema sana, mfano mzuri ni marekani {united states of amerca}, au ujerunmani, kinacho nishawishi zaidi ni ukubwa wa bara letu, yaani bara la pili kwa ukubwa duniani, wingi wa rasilimali zetu na uadimu wake kupatikana katika mabara mengine,vipaja vya watu wetu vinavyotumika kote ulimwenguni kwa faida ya nchi zao, roho za upendo wa kweli na ukarimu tulizonazo { ni kweli katika hili mapungufu yapo lakini yanarekebishika} hivi hatuioni siri hii iliyo wazi mbele yetu kuwa maendeleo ya haraka ya muafrika hayawezi kuletwa na nchi moja moja bali muunano wenye nguvu ya pamoja? sina haja ya kuwakumbusha waasisiwaliotangulia kwani najua mnawajua, yangu nui hayo tuuuuuuuu!
 
nice story...."vipaja" fanyia kazi hapo mkuu kabla jamii haijakuelewa vibaya.
 
naona ka siyo mahali pake hapa ungepeleka jamii intelligence au jukwaa la siasa!
 
Kaeleweka typing error ata kwenye magaazeti zinatokea ila ujumbe umefika.
 
Swala la afrika kuungana lilikua big idea ila linakwamishwa na mambo yafuatayo: 1/urafi wa madaraka kwa viongozi wetu 2/ukosefu wa umoja na mshikamano kwa viongozi na waafrika kwa ujumla 3/nchi za magharibi kuingilia nchi zetu kisiasa na kiuchumi 4/vita vya sisi kwa sisi ndani ya nchi zetu 5/kukosekana kwa demokrasia ya kweli na siasa safi 6/uchumi tegemezi. Nk, sasa nini kifanyike ili tuweze kufiki lengo la kuwa na nchi moja ya afrika kama ilivyo asisiwa na kiongozi wetu shupavu na mwenye ujasiri hayati "KWAME NKRUMAH"?
 
Back
Top Bottom