Kwa mtazamo wangu Thabo Mbeki asingeweza kupata hii Prize kwa sababu kubwa mbili.
Moja rekodi yake kuhusu HIV/AIDS ilikuwa na doa hasa pale aliposhikilia kwamba haukuwa ugonjwa ila ni jambo la kusadikika. Mtazamo huu iliifanya serikali yake kuchelewa kutoa madawa ya kupunguza makali ya (ARVs) HIV/AID S na hivyo kupelekea watu wengi kufa. Mbeki hakuonyesha uongozi bora kwa hili.
Pili ni kwamba Mbeki alitoka madarakani katika hali ya utata. Ingawa alijihudhuru lakini kimsingi alitolewa (he was recalled) na chama chake ANC. Kwa sasa Mbeki ni "black sheep" katika ANC. Tuzo ya Mo Ibrahim ni ya kisiasa. Kamati ingempa tuzo hii ANC na serikali yake wangejisikiaje? Wangeibeza sana. Kamati imeona mbali kwa kutompa Mbeki na hivyo kuepuka controversy za kisiasa.
Sijui kwa nini Rais John Kufour hakupewa. Tusubiri tuone.