African Super League inaanza October

African Super League inaanza October

The Genius

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
822
Reaction score
2,095
Rais wa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) Patrice Motsepe amethibitisha kuwa michuano ya African Super League itaanza kutimua vumbi mwezi Oktoba mwaka huu na kuongeza kwamba kutakuwa na jina jipya kwa ajili ya michuano hiyo ili kuvutia wadhamini zaidi.

Ikiumbukwe Mnamo Novemba 29, 2019, CAF ilitangaza rasmi kuanzishwa kwa African Super League ikiwa na lengo la kuongeza mapato makubwa ya kifedha yanayotarajiwa kuzidi dola milioni 100 ambazo zitatumika kuboresha miundombinu na kukuza mchezo huo barani Afrika.

Akizungumzia sababu za michuano hiyo kubadilishwa jina Motsepe amesema baadhi ya Wadhamini wakubwa wamesema historia ya Super League barani Ulaya haikuwa nzuri na kubainisha kuwa jina Super lina maana hasi kwenye soka.

“Tunaweza kubadili jina, lakini kitakachofanyika Oktoba ni uzinduzi tu huku tukiendelea kutumia jina la 'African Super League' mpaka pale tutakapolinadili”

Awali michuano hiyo ilipangwa kuhusisha timu 24 katika makundi ya timu nane lakini katika uzinduzi Super League itaanza kwa kundi moja la timu 8 ambazo ni Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini), Al Ahly (Misri), Petro de Luanda (Angola), TP. Mazembe (DR Congo), Horoya (Guinea), Wydad Atheltic Club (Morocco), Simba SC (Tanzania) na Esperance de Tunis (Tunisia).

CAF ilitangaza kuwa mshindi wa michuano hiyo atapata kitita cha dola milioni 11.5 huku kila timu shiriki itatia kibindoni kitita cha dola milioni 2.5.
 
Kwa msiojua ni kwamba kutakua na timu moja mualikwa ili kuvutia wadhamini..na hapo kolowizards ndipo mtakapolia kilio Cha gubu
 
Haya timu kubwa mbumbumbu fc isiyo na makombe tumewasikia.

Ila Yanga ni timu mdogo yenye makombe yote ya ndani na wachezaji wanne wa kikosi Cha kwanza Taifa Stars Nondo, Bacca, Mudathir ña Job, Simba timu kubwa duniani ina mmoja Kibu tu anaeañza Stars! Huko benchi kumejaa Yanga tu. Yule mpemba Fei angetulia Yanga angeongeza idadi wakawa 5 na Kibu angeanzia benchi huko Taifa Stars ingekuwa Yanga 5 - Simba 0! Vijana wa Utopoloni wanaenda na mwewe kukiwasha Afcon hapo vipi Makolo toeni comments!

Tunaamini Fei atajifua na kurudisha kiwango chake na kumaliza kazi ya kuondoa magalasa ya Makolo fc Taifa Stars wametufelisha sana!
 
Mbona hapo haijaelezewa Yanga hata sehemu moja wala idadi ya makombe na wachezaji?Kwani utopolo mlilogwa na nani huyo aliyekufa?🤪🤪🤪🤪
 
Ndio maana dp world wanaitaka Tanganyika maana badala ya kujadili Hoja iliyoko mezani watu wameanza kujadili yanga haipo mara ni timu ndogo.
 
Back
Top Bottom