Afrika hoyee, mwanahabari alipokezwa kichapo cha mbwa na mapolisi Tanzania

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
32,408
Reaction score
50,809
Police+pic.jpg

Kufuatia Tukio la kushambuliwa kwa kupigwa kwa mwandishi wa habari lililozidi kushika kasi na kukemewa na viongozi na taasisi mbalimbali nalo jeshi la polisi ambalo ni mtuhumiwa wa kwanza kutokana na kuonekana baadhi ya askari wake wampiga mwandishi huyo kupitia kamanda wa polisi wa kanda maalum Lazaro Mambosasa amelaani tukio hilo

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
TAARIFA KUHUSU PICHA YA VIDEO INAYOSAMBAA MTANDAONI YA KUPIGWA MWANDISHI WA HABARI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es salaam linalaani vikali tukio linalosambaa mtandaoni la kupigwa kwa mwandiishi wa habari wa WAPO Redio aitwaye SILLAS MBISE tukio lililotokea Tarehe 08.08.2018 siku ya mechi kati ya SIMBA vs ASANTE KOTOKO ya nchini Ghana, ambayo siku hiyo lilikuwa tukio la kuazimisha siku ya SIMBA(Simba day).
Aidha Polisi kanda maalum imeanza uchunguzi wa tukio hilo kwa kufungua jalada la uchunguzi wa picha ya video hiyo inayosambaa inayoonesha askari wa Polisi na mwandishi huyo wa habari ili kubaini ukweli.
Hiyo inaenda sambamba na kumtaka mtendewa wa kosa hilo la kupigwa kutoa taarifa kituo cha Polisi ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa. Kwani mtu yeyote anatakiwa kutoa malalamiko yake pale anapoona ametendewa vitendo ambavyo ni kinyume cha sheria.
Sambamba na hayo Polisi jukumu lake kuu ni kulinda usalama wa raia na mali zao na si kuwapiga raia walitenda kosa ambao hawajakataa kutii sheria ya kukamatwa.

L.B. MAMBOSASA– SACP
KAMANDA WA POLISI KANDA MAALUM
DAR ES SALAM.
10.08.2018

Jeshi la Polisi Nalo Lalaani Tukio la Kupigwa kwa Mwandishi wa Habari - BonGossip - Bongo Gossip - Udaku Hardcore
 
Kama ushahidi wa video upo wanangojea nini?. Ama ni zile ngonjera za kawaida?. Wakaulize yule jamaa wetu wa hapa aliponaswa hadharani kwa ushaidi wa video akimdhulumu yule bibi. Ilibidi ikaishie kwa mkurugenzi mkuu wa mashtaka ya umma aliye amrisha kukamatwa kwake. Tunapoongea saa hii yuala ndondo mbichi kwa miaka kumi na mbili ijayo.
 
Tumeambiwa kwamba akishashiba majani hayo hapo ataona ulimwengu wote ameutia mfukoni mawke (.World in my pocket)
 
Huyo ni wa chadema ni sawa tu, isitoshe kila stori ina pande 2!
 
Former haven of peace ndio sasa wameingia enzi zile Kenya tuling'ang'ania kupata the 2nd Liberation, the 90s.
 
Huyo ni wa chadema ni sawa tu, isitoshe kila stori ina pande 2!
Sio vema sana kushabikia upumbavu hata kama umefanywa na mzazi wako. Siasa isitufanye tuwe maadui mkuu, watanzania wote ni ndugu bila kujali itikadi zetu za vyama, dini n.k. Tusishabikie ubaguzi kwani una madhara kwetu na uzao wetu pia.
 
Siwapendi chadema na siwezi kubadilika ni hivyo tu!
 
Mkuu, kutompenda mtu haina maana ufurahie mateso yake. Watanzania milioni 50 hatuwezi kufikiri sawa, kutofautiana ni lazima. Simamia tu haki ijapokuwa huwapendi. Mm binafsi siwapendi wanasiasa karibu wote maana ni waongo, sipendi CCM na pia sipendi CHADEMA ila wapo watu nawapenda ndani ya CCM na pia wapo watu nawapenda ndani ya CHADEMA. Kwangu mimi Taifa kwanza.
 
Whatever man!
 
Usimweleweshe huyo mpumbavu
 
Back
Top Bottom