Afrika kilio: Kwanini hakuna mwarabu anayejiita Masawe, Chacha wala Mwakitabu?

Mwabhleja

JF-Expert Member
Joined
Jan 27, 2016
Posts
1,351
Reaction score
2,061
Hakuna...hakuna...hakuna mwarabu mwenye kujifaharisha kwa majina Yetu.

Mwarabu wa kuitwa Masanja, Chacha,Masawe au Mwakitabu hayupo. Hata wale waarabu ndugu zetu wa Puge kule Nzega, au wale walima tikiti wa Choma kile Igunga, Au wale wavizia madini kule kule Kakola kwenye UKIMWI. Hata wale wa Dabaga, Kitanzini mpaka Mwangata kule Iringa hawataki kuitwa Haule,Mkwawa wala Mnyalu.

Nakwambia hivi, hawana muda wa kujifaharisha kwa majina Yetu.

Achana na hao.
Twende kwa wale wa bara ulaya, hapa kwetu utakutana na kina Joni wengi, kina Paulo ndiyo usiseme na kina Job wamejaa wengi wangekuwa senene kule Uhayani jirani na mto Ngono tungejaza gunia 463794000.

Lakini mbona wao hatuwasikii kujiita mkude, Ntinginya, Mgosi, rutashobya wala Sekwao. Wakati sisi tukijitahidi walau hata kama MTU anaitwa Subiraga walau anajiita Suby ili litamkike kikwao lakini wao hata kama mtu anaitwa Trump hawawezi kutohoa kutambua uwepo wetu walau ajiite Mwatulampu Mara moja moja misibani kama ameshindwa kutweet.

Kitu gani kimetudhuru?
Ndiyo maana mvua hazinyeshi kwa misimu ya kueleweka kama zamani. Kwa utafiti wangu, kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo wanaojitambua kwa majina yao ya kiasili wanavyopungua.

Hii imesababisha pia kupungua kwa kipenyo cha utofauti wa kijinsia. Kwa mfano utakuta mwanamke anaitwa Antonia wakati huo huo mwanaume anaitwa Anthony. Ushoga na usagaji Mara nyingine huanzia kwenye kuzoea utofauti finyu baina ya mwanamke na mwanaume. Ilikuwa hivi; tulikuwa na Koku Vs Muganyizi, Maranya Vs Bhoke, Tarimo Vs Manka, Atuganile Vs Mwakyembe n.k

Ukoloni mamboleo mpaka kwenye majina? Kwahiyo tuna Makinikia ya majina?
Yaani tumerogwa akili na kukubali kutawaliwa hata kwa kile tunachokiishi kila siku?

Siku gani itapita hujamuita MTU jina?

Hatimaye tunaitana kwa majina ya kigeni, tunafikiri kama wageni, tunaabudu kama wageni, tunavaa kama wageni, tunataka mwonekano kama wa wageni na tunaishi kwa matumaini ya kuishi kama wageni siku moja mbeleni.Hatuwezi kubarikiwa...sisi mfano wetu ni wageni au Mungu/Miungu?

Ndugu zangu tumepotea!
Ng'ombe aliyepotea marishoni hujikongoja kurudi nyumbani. Twende kwetu Afrika...hatujachelewa!

Twende na Dada zetu wenye sura halisi za bibi zao, wenye mavazi yenye nembo ya utamaduni wetu. Twende na vijana wetu huku tukiwapandisha mlegezo, tuwaandae kuwa kina Morani,Mnyalu,Mgosi,Nnyambala na Ngosha.

Tuwaimbie nyimbo za kutunza familia siyo kutunza simu. Wataelewa na mwisho wa siku tutaokoa kizazi kizima.

Tutakuwa na watu wanaojipenda, wanaopenda vya kwao na hatimaye utamaduni wao utapelekea Mapinduzi ya viwanda. Tutapata soko LA chain zilizoandikwa Kambarage badala ya hizi zilizoandikwa NY na vitu vingine vingi.
NATAMANI MNYORORO HUU UWE HIVI
Mwafrika Huru~Mwafrika Mtumwa~Mwafrika Mtawaliwa~Mwafrika Mtawaliwa Huru~Natamani turudi kwa MWAFRIKA HURU!

Nini maoni yako?
 
Mwarabu ni kiumbe cha kishenzi kuwai kutokea duniani

Kiumbe aliyestaarabika duniani ni mwafrika tu
 
Pamoja na hayo yote, kwanini mwarabu anathamini vya kwake kuliko afanyavyo mwafrika mweusi?
Si kwamba kuna fasiri ya umajumui wa kiafrika unayosahaulika kwenye ustaarabu wetu?
 
Joseverest, mi watoto wangu ni wawili mmoja nyamaghaka, mwingine mwita
 
Pamoja na hayo yote, kwanini mwarabu anathamini vya kwake kuliko afanyavyo mwafrika mweusi?
Si kwamba kuna fasiri ya umajumui wa kiafrika unayosahaulika kwenye ustaarabu wetu?
Kuthammini hata sisi tunathamini mfano mzuri ni wazazi wako wasinge thamini u africa wao usingezaliwa

Swala ni kwamba mwarabu ni mshenzi
 
Majina yenyewe ya kiarabu machachee, ukienda Shule quite juma Abdul wananyanyuka watoto 14, lakini zunguka Tanzania nzima pombe Magufuli ni mmoja tu
 
Hakuna...hakuna...hakuna mwarabu mwenye kujifaharisha kwa majina Yetu.

Mwarabu wa kuitwa Masanja, Chacha,Masawe au Mwakitabu hayupo. Hata wale waarabu ndugu zetu wa Puge kule Nzega, au wale walima tikiti wa Choma kile Igunga, Au wale wavizia madini kule kule Kakola kwenye UKIMWI. Hata wale wa Dabaga, Kitanzini mpaka Mwangata kule Iringa hawataki kuitwa Haule,Mkwawa wala Mnyalu.

Nakwambia hivi, hawana muda wa kujifaharisha kwa majina Yetu.

Achana na hao.
Twende kwa wale wa bara ulaya, hapa kwetu utakutana na kina Joni wengi, kina Paulo ndiyo usiseme na kina Job wamejaa wengi wangekuwa senene kule Uhayani jirani na mto Ngono tungejaza gunia 463794000.

Lakini mbona wao hatuwasikii kujiita mkude, Ntinginya, Mgosi, rutashobya wala Sekwao. Wakati sisi tukijitahidi walau hata kama MTU anaitwa Subiraga walau anajiita Suby ili litamkike kikwao lakini wao hata kama mtu anaitwa Trump hawawezi kutohoa kutambua uwepo wetu walau ajiite Mwatulampu Mara moja moja misibani kama ameshindwa kutweet.

Kitu gani kimetudhuru?
Ndiyo maana mvua hazinyeshi kwa misimu ya kueleweka kama zamani. Kwa utafiti wangu, kadri siku zinavyosonga mbele ndivyo wanaojitambua kwa majina yao ya kiasili wanavyopungua.

Hii imesababisha pia kupungua kwa kipenyo cha utofauti wa kijinsia. Kwa mfano utakuta mwanamke anaitwa Antonia wakati huo huo mwanaume anaitwa Anthony. Ushoga na usagaji Mara nyingine huanzia kwenye kuzoea utofauti finyu baina ya mwanamke na mwanaume. Ilikuwa hivi; tulikuwa na Koku Vs Muganyizi, Maranya Vs Bhoke, Tarimo Vs Manka, Atuganile Vs Mwakyembe n.k

Ukoloni mamboleo mpaka kwenye majina? Kwahiyo tuna Makinikia ya majina?
Yaani tumerogwa akili na kukubali kutawaliwa hata kwa kile tunachokiishi kila siku?

Siku gani itapita hujamuita MTU jina?

Hatimaye tunaitana kwa majina ya kigeni, tunafikiri kama wageni, tunaabudu kama wageni, tunavaa kama wageni, tunataka mwonekano kama wa wageni na tunaishi kwa matumaini ya kuishi kama wageni siku moja mbeleni.Hatuwezi kubarikiwa...sisi mfano wetu ni wageni au Mungu/Miungu?

Ndugu zangu tumepotea!
Ng'ombe aliyepotea marishoni hujikongoja kurudi nyumbani. Twende kwetu Afrika...hatujachelewa!

Twende na Dada zetu wenye sura halisi za bibi zao, wenye mavazi yenye nembo ya utamaduni wetu. Twende na vijana wetu huku tukiwapandisha mlegezo, tuwaandae kuwa kina Morani,Mnyalu,Mgosi,Nnyambala na Ngosha.

Tuwaimbie nyimbo za kutunza familia siyo kutunza simu. Wataelewa na mwisho wa siku tutaokoa kizazi kizima.

Tutakuwa na watu wanaojipenda, wanaopenda vya kwao na hatimaye utamaduni wao utapelekea Mapinduzi ya viwanda. Tutapata soko LA chain zilizoandikwa Kambarage badala ya hizi zilizoandikwa NY na vitu vingine vingi.
NATAMANI MNYORORO HUU UWE HIVI
Mwafrika Huru~Mwafrika Mtumwa~Mwafrika Mtawaliwa~Mwafrika Mtawaliwa Huru~Natamani turudi kwa MWAFRIKA HURU!

Nini maoni yako?

Mimi nimeanza na watoto wangu.
1. Mboka
2. Atuganile
3. Ipyana.
Nimemshangaa Harrison Mwakyembe, aliyoyaandika kwenye riwaya ya PEPO YA MABWEGE sicho anachokiishi.
 
Back
Top Bottom