Afrika Kusini inapeleka silaha na wanajeshi Congo

Afrika Kusini inapeleka silaha na wanajeshi Congo

Shing Yui

JF-Expert Member
Joined
Aug 8, 2015
Posts
15,168
Reaction score
38,049
Afrika Kusini imepeleka wanajeshi zaidi na zana za kivita nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo mnamo siku za hivi karibuni.

DR Kongo |  M23-Soldaten in Goma
Wapiganaji wa M23 wanaonekana huko Goma Februari 6, 2025 kwa ajili ya mkutano wa hadhara ulioitishwa na kundi hilo lenye silaha.Picha: ALEXIS HUGUET/AFP via Getty Images

Hatua hiyo inatekelezwa ikiwa ni wiki kadhaa tangu askari wake 14 walipouliwa kwenye makabiliano na waasi wa M23 mashariki mwa taifa hilo. Hayo yameelezwa na vyanzo kadhaa vya kisiasa na kidiplomasia vilivyozungumza na shirika la habari la Reuters.

Mbunge mmoja wa Afrika Kusini amesema wamearifiwa kwamba takribani wanajeshi 700 hadi 800 wamepelekwa Lubumbashi.

Afrika Kusini inaiunga mkono serikali ya Kongo kwenye mapambano dhidi ya waasi wa M23 ambao sasa wanadhibiti mji muhimu wa Goma mashariki wa nchi hiyo na wametishia kusonga mbele na kukamata maeneo makubwa zaidi.

Hayo yanaripotiwa wakati hali ya utulivu imeshuhudiwa kwa siku ya pili mfululizo mashariki mwa Kongo baada ya wiki kadhaa za makabiliano kati ya vikosi vya serikali na waasi wa M23.

Mfanyakazi mmoja wa uwanja wa ndege akizungumza bila kutajwa jina amesema ndege za kijeshi zimepelekwa, huku ndege za mizigo zinatua mara kwa mara zikileta silaha
 
Tokea JF iwe na watoto wa elfu mbili imekua kama Facebook sasa...
JF ilianzishwa mwaka 2006, na tulishiriki. Nitajie ID yako ya Zama hizo nami nitataja yangu, tuone mgeni jamvini ni Nani? Tutakumbushana na matukio yetu pamoja kama JF founders
Screenshot_2025-02-11-21-08-07-75.png
 
Back
Top Bottom