Afrika Kusini: Mahakama yamhukumu Kocha wa timu ya Taifa Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kwa makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia

Afrika Kusini: Mahakama yamhukumu Kocha wa timu ya Taifa Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kwa makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
MAHAKAMA ya Afrika Kusini imemhukumu kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na makossa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia, alisema mwendesha mashtaka juzi Jumanne.

Micho aliripotiwa kufanya kosa hilo mwaka jana wakati alipokuwa akiinoa Zambia.

“Mapema asubuhi (juzi Jumanne), mahakama ya Port Elizabeth ilimkuta na hatia kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia, Milutin Sredojevic, katika makosa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia,” ilifichua taarifa ya Mamlaka ya Taifa ya Mashtaka (NPA).

Hukumu ya kifungo cha miaka mitatu inaweza kugeuka na kuwa cha miaka mitano kama atafanya kosa jingine la aina hiyo.

Tukio hilo lilitokea Desemba 2020 katika michuano iliyofanyika katika mji wa Gqeberha, Afrika Kusini ambao zamani ulifahamika kama Port Elizabeth.

Mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 39 alikuwa akifanya kazi ya kugawa kahawa uwanjani hapo, ndipo alipomuuliza Micho kama atahitaji sukari kwenye kahawa yake, ambapo Mserbia huyo alisema “hapana na kisha kuongeza kwamba anataka sukari ya aina nyingine, akionyesha kidole kwenye sehemu za siri za mwanamke huyo,” ilibainisha NPA.

1634809670101.png
 
MAHAKAMA ya Afrika Kusini imemhukumu kocha wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin “Micho” Sredojevic kifungo cha miaka mitatu baada ya kukutwa na makossa mawili ya unyanyasaji wa kijinsia, alisema mwendesha mashtaka juzi Jumanne...
Duh....
 
Nafikiri Micho alikuwa kwenye utani.
Au pengine muuza kahawa alitafuta pa kutokea.

Nadhani mahakama ingeweza kutumia muda huo kutatua case za ufisadi na uhujumu uchumi kuliko kupoteza muda kudeal na mambo ambayo ata balozi wa nyumba kumi angeweza kulitatua.
 
Nafikiri Micho alikuwa kwenye utani.
Au pengine muuza kahawa alitafuta pa kutokea.

Nadhani mahakama ingeweza kutumia muda huo kutatua case za ufisadi na uhujumu uchumi kuliko kupoteza muda kudeal na mambo ambayo ata balozi wa nyumba kumi angeweza kulitatua.
That is our mindset. Yaani akinyanyaswa mwanamke unakuwa utani. Utamtaniaje mtu ambaye humfahamu tena matani ya nguoni. Katika sheria, "you cannot pick and choose". Hiyo ni sheria ya jinai na anatakiwa kuifungwa tena kulipa faini. Hivi angemwambia mama au dada yako hayo, wewe ungechekelea na kuuita utani! Just place people you love in the scenario and le me know how you feel.
 
Wataalam waje watuambie ataenda jela au itakuaje maana yupo kazin Uganda au Uganda itamkabidhi kwa SA
Hapo inamaana trial yake imeendeshwa 'in absentia' na kuhusu kukabidhiwa na Uganda (extradition) inategemea na sheria za extradition za Uganda zinasemaje.

Vinginevyo ni kuwa huko SA Micho atakuwa most wanted na siku akikanyaga tu anakamatwa anawekwa ndani.
 
Huku kocha katudhalilisha kibinadamu kwa kutuita manyani na hakutiwa hatiani
 
Back
Top Bottom