AFRIKA KUSINI: Matamasha ya Kofi Olomide yafutwa, atuhumiwa kwa kumbaka mnenguaji wake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Matamasha mawili ya mwanamuziki Nguli wa miondoko ya Rumba nchini DRC Kofi Olomide yamefutwa huko nchini Afrika Kusini kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji hivi karibuni dhidi ya mnenguaji wake.

Olomide mwenye umri wa miaka 62 ambae jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alitarajiwa kuwa na tamasha katika ukumbi wa Gallagher Convention Centre nje kidogo ya jiji la Johannesburg June 28 pamoja na lingine katika ukumbi wa the Shimmy Beach Club huko Cape Town siku mbili baadaye.

Baada ya kampeni ilioendeshwa kwenye mitandao ya kijamii, hatimae mkurugenzi wa ukumbi wa Gallagher Convention Center, Charles Wilson amesema katika taarifa yake kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Wakati huo, huo ukumbi wa Shimmy Beach nao umetangaza mapema kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Mwezi Machi mahakama ya jijini paris ilimuhukumu Olomide kifungo cha miaka 2 baada ya kesi ambayo hata hivyo hakuhudhuria.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimfutua tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanenguaji wengine 3 nyumbani kwake jijini Paris mwaka 2002-2006.

Olomide aliwahi kutiwa mbaroni kwa muda mfupi mwaka 2016 baada ya kumpinga mnenguaji wake jijini Nairobi nchini Kenya ambapo alihukumiwa kifungo cha mieizi mitatu jela mwaka 2012 baada ya kumpiga mtengenezaji wa muziki wake.

Polisi nchini Zambia inamtafuta Koffi Olomide kwa kosa la kumpiga mpiga picha rais wa Rwanda jijini Lusaka nchini Zambia mwaka 2012.
 
Matendo ya kofi ni kielelezo cha manyanyaso wanayo yapata wasaidizi wetu sisi Waafrika.

Mtu kumbaka na kumpiga housegirl anaona ni kitu cha kawaida.

Kuna ma bazazi yanawaharibu watoto wa kiume wanaowafanyia kazi. Unachukulia shida na matatizo yake kumlawiti ukijua hana ujanja wa kukataa.
 
Matamasha mawili ya mwanamuziki Nguli wa miondoko ya Rumba nchini DRC Kofi Olomide yamefutwa huko nchini Afrika Kusini kutokana na kukutwa na makosa ya ubakaji hivi karibuni dhidi ya mnenguaji wake.

Olomide mwenye umri wa miaka 62 ambae jina lake halisi ni Antoine Agbepa Mumba alitarajiwa kuwa na tamasha katika ukumbi wa Gallagher Convention Centre nje kidogo ya jiji la Johannesburg June 28 pamoja na lingine katika ukumbi wa the Shimmy Beach Club huko Cape Town siku mbili baadaye.

Baada ya kampeni ilioendeshwa kwenye mitandao ya kijamii, hatimae mkurugenzi wa ukumbi wa Gallagher Convention Center, Charles Wilson amesema katika taarifa yake kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Wakati huo, huo ukumbi wa Shimmy Beach nao umetangaza mapema kwamba tamasha la Koffi Olomide limefutwa.

Mwezi Machi mahakama ya jijini paris ilimuhukumu Olomide kifungo cha miaka 2 baada ya kesi ambayo hata hivyo hakuhudhuria.

Hata hivyo mahakama hiyo ilimfutua tuhuma za unyanyasaji wa kingono dhidi ya wanenguaji wengine 3 nyumbani kwake jijini Paris mwaka 2002-2006.

Olomide aliwahi kutiwa mbaroni kwa muda mfupi mwaka 2016 baada ya kumpinga mnenguaji wake jijini Nairobi nchini Kenya ambapo alihukumiwa kifungo cha mieizi mitatu jela mwaka 2012 baada ya kumpiga mtengenezaji wa muziki wake.

Polisi nchini Zambia inamtafuta Koffi Olomide kwa kosa la kumpiga mpiga picha rais wa Rwanda jijini Lusaka nchini Zambia mwaka 2012.
mpiga picha rais wa Rwanda jijini Lusaka nchini Zambia mwaka 2012." hapa jombaa ulikua unamaanisha kitu gani ?
 
Nimefurahi sana baada ya kupigwa ban kwa huyu mzee. Sababu ni hizi:
1. Nimegundua huyu mzee hana uchungu wowote na Congo na Wacongo wezake. Mfano: anatumia muda mwingi kujitanabaisha kama si raia wa Congo isipokuwa ni Mfaransa mweusi
2. Pamoja na utajiri mkubwa alionao kashindwa hata kununua boti hata ya mkopo kuwasaidia Wacongo wanaozama na kufa kwenye mto Congo kila kukicha. Tanzania tuna matajiri wa kujivunia kama AZAM Bhakharessa na boti zake za Dar to Zenj.
3. Wakati wanamziki wa Congo wakijikusanya kwa ajili ya mazishi ya mwanamziki Lutumba Simaro mzee asiye na busara Koffi katimkia Paris kula bata na bintie Didi Stone.
4. Moise Katumbi mmiliki wa TP Mazembe pamoja na kukataliwa kurudi DRC wakati wa utawala wa raisi aliyemaliza muda wake aliamua kukaa Afrika na sehemu aliyochagua ni Afrika Kusini
NB: Astaafu mziki na akaishi huko kwao Ufaransa
 
Back
Top Bottom