Afrika Kusini: Wezi wavamia nyumba ya Waziri wa zamani na kupora iPhone, TV na Laptop

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Aliyekuwa Waziri wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Naledi Pandor, pamoja na familia yake, walivamiwa na kushikiliwa kwa mitutu ya bunduki na majambazi wenye silaha nyumbani kwao mkoani Pretoria, usiku wa kuamkia Mei 23, 2026.

Msemaji wa Jeshi la Polisi Kitaifa, Brigedia Athlenda Mathe, aliiambia News24 kwamba wanaume watatu waliokuwa wamejifunika nyuso zao kwa kofia za masks (balaclavas) walivamia nyumba ya familia hiyo majira ya saa tatu na nusu usiku

Majambazi hao walitoroka baada ya kupora gari la familia hiyo, simu aina ya iPhone, runinga (TV), pamoja na kompyuta mpakato (laptop).

Hata hivyo, gari hilo lilikuja kupatikana baadaye likiwa limetelekezwa katika eneo la Mamelodi Mashariki.


Waziri wa zamani wa Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano wa Afrika Kusini, Naledi Pandor
​

Source: News 24
 
uhalifu kama huo ni jambo la kawaoda sana Africa Kusini
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…