Afrika Kusini yakataa kuwa mwenyeji wa wakimbizi wa Afghanistan

Afrika Kusini yakataa kuwa mwenyeji wa wakimbizi wa Afghanistan

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Afrika Kusini imesema haiwezi kuchukua wakimbizi kutoka Afghanistan licha ya ombi.

"Afrika Kusini tayari ni makazi ya idadi kubwa ya wakimbizi na imebanwa kushughulikia mahitaji yao," Idara ya Uhusiano wa Kimataifa ilisema katika taarifa yake.

Ilisema ilikuwa imeombwa kuchukua wakimbizi ambao walikuwa nchini Pakistan kwa nchi wanazopitia.

Lakini ilisema haikuwa katika nafasi ya kukubali "wakimbizi watahudumiwa vyema kwa kubaki Pakistan, nchi yao ya kwanza ya kuwasili".

Baadhi ya nchi nyingine kama Rwanda na Uganda tayari zimekubali kuwa wenyeji wa wakimbizi wa Afghanistan wakati wanasubiri kupelekwa katika nchi nyingine.
 

Attachments

  • 1630572458047.gif
    1630572458047.gif
    42 bytes · Views: 5
Marekani ndie aliivuruga hii nchi na kuzalisha wakimbizi so abebe yeye hilo jukumu.

Apeleke wakimbizi wote us
 
Kwa nini wasiwape hifadhi katika nchi zinazopakana na Afghanistan ? Hawa siyo wa kupokea kirahisi, baada ya muda huanzisha mambo yaleyale yaliyowafanya kuwa wakimbizi.
Chunga Sana kinywa chako maana hayo ni matapishi
 
Kwanza kwa nini wanaikimbia nchi yao wenyewe, watakimbiaje sheria za kiislamu ilhali na wenyewe ni waislamu?

Na tena hawa watu wanashangaza sana, piga ua hawataki kwenda kwenye nchi za kiislam.

Inaonekana hizi zinazojiita mataifa ya kiislamu raia wamebanwa mno kiasi kwamba wakipata mwanya tu hakuna mtu anayeweza kubaki kwenye hizo nchi. Binadamu aliumbwa awe huru sio kuchungwa kila saa kama ng'ombe.
 
Jamaa kawasababishia ukimbizi halafu akijimwambafai anawahamisha halafu Tena anawatafutia pakwenda na sio huko ughaibuni tena bali nchi za kiafrika
 
Back
Top Bottom