#COVID19 Afrika Kusini yalegeza masharti ya kupambana na Coronavirus

#COVID19 Afrika Kusini yalegeza masharti ya kupambana na Coronavirus

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa ametangaza cheti kipya cha chanjo ya COVID-19 ambacho amesema kitarahisisha kusafiri na kuhudhuria matukio ambayo yanahitaji uthibitisho wa chanjo.

“ Wizara ya Afya hivi karibuni itaanza kutoa cheti cha chanjo cha COVID-19 ambacho kitaonyesha uthibitisho rasmi wa chanjo.

Cheti hicho kitatumika kuwezesha safari na mikusanyiko na shughuli nyingine ambazo zinahitaji uthibitisho wa chanjo,” ameeleza.

Ramaphosa pia amelegeza masharti ya ndani dhidi ya janga la corona, ikiwemo kupunguza muda wa masharti ya kutoka nje, ameondoa marufuku ya uuzaji wa pombe majira ya usiku, na kuruhusu mikusanyiko mikubwa.

Amesema serikali ina mpango wa kutoa dozi za chanjo 250,000 kila siku hadi katikati ya mwezi Desemba.
 
Pole yao sana...

Tanzania hatujawahi kua na corona...
 
Sisi huku hatujali kuhusu masharti ya kupambana na corona tulishalegeza masharti kitambo, siye tuko busy na hivi vichanjo milioni moja tukiamini kuwa ndio vitasaidia kutukinga na corona pamoja na kuwa hadi sasa tumechanja laki nne tu katika M60.

Tunaendelea vizuri.
 
Back
Top Bottom