Safari Afrika
New Member
- Jun 3, 2023
- 1
- 0
Mwandishi:Safari Afrika
Mfu Afrika na uhuru Bandia, Nasikia huna raha maana machungu umezoa, umechoka kulia na kushoto unaelekea, jua limekuchwa na kivuli chako katu hakikusogea.
Afrika uliye mfu maana umeliwa na siasa,
Nusu mfu wanao kujenga ni vijana na wamezimia kwenye anasa,
Mama afrika ni wewe umefumba macho usione unapo kwenda na ujui utakacho,
Ulisimikwa kama mkuki, ila sasa umegeuka fimbo, sisi kwasisi tunajenga chuki na bado tunaimba wimbo, wewe ni mjinga au shujaa uliye jengwa na wageni wako, ukawafukuza ili ujiongoze peke yako, cha ajabu leo vita imebaki kwako.
Tunasababu za msingi tukitaka kuongea mengi,tunatumia mifano mingi ili kupata ushindi,
Na harufu chafu ya Damu unayoisikia, ni waafrika kama sisi waliokufa bila hatia, njaa changamoto na magonjwa ya sio kwisha, ujinga na umaskini ni adui aliyetushika, mbele tusiende tuone nyuma kuna faa, tuyapinge afrika kuijenga kwa ufasaha.
Mimi na wewe ni nguzo ya afrika bora walijenga babu zetu nasi tutunze cha kwetu, tumezaliwa na mali nyingi ila umaskini umetujaa,na tunakufa maskini kama tulipenda pia,hatuna jambo jema ikiwa wema awezi ishi nasi pia, na hatusogei maana tunazunguka kama pia.
Afrika unarudi kwa kasi na wewe bado unaona unakimbia,walitutawala tukiwa vyema maana ujinga atukuzoea,leo tuna waambia kuhusu sisi ili watusaidie sisi, na tunajua kabisa hawapendi kuhusu sisi, yaani kama tumelogwa au tuna undugu na Ibilisi.
Afrika tuna jifunza kujiogopa na sio kujiamini tena,tuna baki tuna ongopana si kusema ukweli tena,tuna pingana ili nani awe mkubwa, na atutazami mbali tuna ishi kama mbwa.
Elimu ya uongo imedumaza akili zetu, si sifa ila kwani tujifunze kukataa vyetu, wakina dada warembo uzuri ni biashara, wakina kaka wanageuzwa mgongo na hatuoni hii ni hasara?
Kama jua likizama tuna sema ni machweo, basi mwenda kwao sio mtoro ila si hivyo Leo,tume acha nyimbo zetu tuka imba za kwao, wao wakatufuata sisi na sisi tume baki na mshangao,
Kama mfu aliyezikwa katikati ya walio hai, Afrika salamu yangu bado nakusabahi,Tuna jenga kila jema, ila hatu semi kila wema, tuna rumbana kusema nani awe kiongozi na wote hawana sifa njema.
Afrika kama ukisimama juu ya mlima kilimanjaro, uta tazama mataifa mbuga za wanyama na jangwa sahara, pembeni tuna zungukwa na wingi wa mabara wanaotaka kututumia tuwaongoze kama dira, maziwa na mito madini yenye samani, umoja kujituma na tamaduni za samani, furaha iliyopo kujivunia na amani,
Wageni toka mbali wanataka jifunza kwangu,ukarimu ndo usijari kwetu umepata ndugu, nguvu na ushujaa viongozi walio bora,Najivunia umenizaa baraka kwako shujaa, ujapoteza yako asili kwa wingi wasanaa, sauti za busara kwa wazee najivunia, makabila makubwa najivunia kwa ushujaa, shona,hehe,zebe, yoruba mandika,wanyamwezi wamasai bambari toka afrika,
Afrika Historia haikuanza na utumwa, Afrika ni ndoto ya upendo ambayo leo inazimwa, afrika iliyoongozwa na viongozi bora, mashujaa wa uhuru walijenga nguzo imara,Nkwame Nkurumah na Nelson Mandela, Julius kambarage na Thomas Sankara, Tujifunze kuhusu Afrika na weusi tusiupoteze,tusipigane vita ili afrika ipendeze.
Wapi Malcom X au Martin Luther king Junior, Marcus Garvey,au Ahmed Soko Toure, Mungu ibariki afrika Mbariki Jomo kenyata, Tuwafunze watoto viongozi Bora tutapata, ASANTE MUNGU MAANA BADO UNATUPENDA, TUSHIKE MKONO MAANA HATUJUI TUNAPOKWENDA.
Giza na mwanga havina urafiki wa kudumu, kumpenda mtu kwa kigezo cha msaada Afrika hii ni sumu,yawezekana sisi ni wajinga na tumejihukumu, ila ukweli kuongea lugha ya kigeni ili tukubalike kwao ni ibada ya sanamu.
Walipo kuja kwetu Ardhi ilikuwa mali yetu, wakasema tufumbe macho tuombe kusema amen Afrika si mali yetu, elimu ya kitumwa ina mtuma kiongozi wa afrika Kukopa, elimu ya kitumwa inamtuma kiongozi kuwa fisadi na kuongopa,
Wanashika Biblia wana apa na kesho wanaiba, wanajua mungu yule afanyi kazi ndo maana wanampima, Afrika kama kisima kinacho chotwa maji na mchanga, utaalamu wetu wakati wa giza labda ndo maana unaitwa mwanga,
tumesimama tunapigana na mwamuzi ni muanzilishi wa ugomvi tena, tunaamini tutafika mbali ikiwa mwamuzi anatuuzia silaha tena, achoki kuja kukaa kwetu kwa ahadi za viongozi wetu kulindwa vyema.
AFrika wasomi hawasomi kutukomboa, Afrika wasomi wanasoma ili kutukomoa,
Afrika auoni chakula ule ushibe uishinde njaa,ila Afrika unaona chakula kinaiva kisha unaahidiwa utakula kikipoa, mwisho unakabidhiwa vyombo uoshe na uchague ni sahani ipi itakufaa, ukiuliza huna jema maana mwema hufa na njaa.
Tuna nyimbo za taifa, na nyimbo za sifa
Tuna nyimbo za taifa, na zimepoteza sifa
Tuna nyimbo za taifa, huku waimbaji wanakufa, wakiimba nyimbo za taifa
Tuna nyimbo za taifa, zikiimbwa na Rushwa, tuna nyimbo za taifa, viongozi wako tayari kubomoa nyumba ili wazibe ufa.
Afrika isiyo weza kujitegemea, inapotea
Afrika isiyo weza kujikemea, taratibu inajongea, kwenye shimo la utumwa ikisogea, mwisho ni vilio maana wanao tuuza ni wale tulo wapa kula mwisho wakakimbia.
Tuna endesha serikali, zenye siri kali
Ni kweli kama hatujatoka mbali, kila kitu
Kipo shwari,ila mwisho ni uchungu wa hii safari.
Turudi nyuma tukae tujue wapi tulikosea,
Tuwaambie watoto Mkwawa alitawala Tanganyika sio iringa na Mbeya, tuwafundishe kujipenda na maovu kuyakemea, tupate viongozi ambao kimsingi watatu semea kutoka moyoni, sio porojo mabungeni kila siku kuongea,
Siasa ni ugonjwa unao hitaji tiba nani ajitokeze, aturudishe enzi za ufalme mali tuogelee, tulinde tamaduni zetu na maisha tufike uzee, ndoa zidumu tena ili ustarabu wa sasa ustarabike, Afika tunaweza tukibadili mifumo ya kigeni, tuliojaribu kuipenda imetushinda japo hili hatuoni.
ASANTE MUNGU MAANA BADO UNATUPENDA, TUSHIKE MKONO MANA HATUJUI TUNAPO KWENDA.
AFRIKA.

Upvote
0