Kilongwe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2008
- 423
- 116
Wanajamii,nina imani wengi wetu tuna moyo wa kuchangia elimu yetu kwa jamii.
Timu nzima ya AfroIT inahitaji wataalam ambao wana moyo wa kujitolea kuandika makala mbalimbali zinazohusu ICT na teknohama kwa ujumla.
Kwa sasa,hatuna uwezo wa kukulipa kwa kazi hii ila wanajamii wenyewe ndio watakaokulipa.Pia kwa kufanya hivi nina imani unajijengea uzoefu mkubwa wa kufafanua ulichokielewa kwani mada zote huwekwa kwenye AfroIT na mitandao rafiki ambapo mamia ya watu hutembelea na kujisomea.Hivyo utapata changamoto na ari zaidi.
Kitu cha muhimu ni kuwa,hakuna mtu aliyezaliwa na kuanza kukimbia,hivyo usiogope kwakuwa huna uzoefu,uzoefu utaupata ndani ya AfroIT.Binafsi nilianzisha AfroIT pindi nikiwa digrii ya kwanza mwaka wa pili,sikuwa na uzoefu wowote,hii ilitokana na mawazo na upendo wangu kwa jamii kwani watanzania wengi tumekuwa watu wa kulaumu sana,sasa muda ufike tuanze kuonesha ari zetu kwa vitendo.
Muhimu: Kila muandishi ataweza kuingia kwenye timu ya waandishi wa AfroIT na ataweza kupata faida zote za waandishi wa AfroIT zikiwemo kutambulika kama mwandishi wa AfroIT,kuruhusiwa kutumia Logo ya AfroIT,kushiriki katika kila uendelezi wa AfroIT na nyinginezo ambazo zinakuja jinsi siku zinavyosonga mbele.
Mwisho: Tupo njiani katika kukamilisha AfroIT Kisima .Hii ni kitu kama Wikipedia(au Baidu Sayansi) ambayo italenga sana Afrika ya Mashariki(Lugha mama itakuwa ni Kiswahili),AfroIT Kisima itakuwa na kila kitu,sio tu ICT bali hata mambo ya Afya,mazingira,mechanics nk ambapo waandishi na members wote wa AfroIT watakuwa na uwezo wa kuchangia makala,kuhariri nk.Sio tu kuwa na mambo mengi bali pia Wana AfroIT Kisima wataweza kuwa na Social Network kati yao.
Hii ni Phase ya Nne baada ya Phase ya tatu ambayo tunatarajia kuitoa Siku yoyote ya wiki inayokuja.
Kushiriki uandishi tuandikie kwenye webmaster@afroit.com kama una maoni au ushauri basi nenda kwenye AfroIT Forums.
Nyoni
AfroIT Group