Afunga Ndoa na Binti Yake Ili Kupata Pasipoti ya Uingereza

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363

Mzee Jelili Adesanya katika picha yake ya harusi na binti yake Karimotu Adenike Saturday, November 21, 2009 3:58 AM


Ili kumwezesha binti yake aweze kupata viza ya kumruhusu aishi Uingereza na baadae apate 'makaratasi' ya Uingereza, mzee mmoja toka Nigeria mwenye pasipoti ya Uingereza amefunga ndoa na binti yake. Mzee Jelili Adesanya mwenye umri wa miaka 54, mzaliwa wa Nigeria mwenye pasipoti ya Uingereza anafanyiwa uchunguzi baada ya kugundulika kuwa amefunga ndoa na binti yake wa kumzaa.

Mzee Jelili ambaye yupo nchini Uingereza tangia mwaka 1976 anatuhumiwa kufunga ndoa na binti yake Karimotu Adenike na kuishi naye kwa kuzuga kama mke wake ili aweze kupata "makaratasi" ya Uingereza.

Magazeti ya Uingereza yalitoa habari hii yakiambatanisha na picha ya harusi ya Jelili na binti yake wakiwa wameshikana mikono kama maharusi wa kweli.

Taarifa zilizotolewa na karibia magazeti yote ya Uingereza zilisema kwamba Jelili alifunga ndoa ya bomani na binti yake nchini Nigeria tarehe 29 mwezi mei mwaka 2007 na baada ya hapo aliomba viza ya miaka miwili ya ndoa kumwezesha "Mke wake" (binti yake) aishi Uingereza. Alipewa viza hiyo mwezi oktoba mwaka huo huo.

Baba na mwanae walikuwa wamepanga kuwa baada ya miaka miwili, binti yake atapata sheria za Uingereza za kumruhusu kuishi milele Uingereza na hivyo ataivunja ndoa yake na baba yake na kisha atafunga ndoa tena lakini safari hiyo itakuwa na mumewe wa kweli anayeishi Nigeria ambaye amezaa naye watoto wanne.

Mpango huo umeingia chachu baada ya mdaku mmoja asiyejulikana wa nchini Nigeria kuripoti ubalozini, wizarani mpaka kwa mawaziri kuwa mzee huyo amefunga ndoa na binti yake.

Taarifa zilisema kwamba wizara ya mambo ya ndani ya Uingereza ilitaarifiwa suala hilo na mdaku huyo miaka miwili iliyopita lakini haikuchukua uamuzi wowote.

Mdaku huyo awali alituma barua ubalozi wa Uingereza nchini Nigeria akiwataarifu suala hilo akiambatanisha majina yao, anuani zao, namba za pasipoti zao mpaka picha ya harusi yao.

Baada ya kuona hamna hatua yoyote iliyochukuliwa, februari mosi mwaka huu mdaku huyo aliamua kuwatumia email waziri wa mambo ya ndani wa Uingereza wa wakati huo, Jacqui Smith na mawaziri Vernon Coaker na Phil Woolas lakini mawaziri hao nao hawakuchukua hatua yoyote.

Taarifa zaidi zilisema kwamba Adenike alibadilisha umri wake kwenye pasipoti yake kwa kujiongezea miaka 10 zaidi ili kusiwe na tofauti kubwa ya umri kati yake na baba yake. Adenike hivi sasa ana umri wa kwenye miaka ya 30 na ushee.

Taarifa zaidi zilisema kwamba hata harusi yao iliyofanyika Nigeria ilifanyika kwa kuzuga kwa kukodisha wahudhuriaji wa harusi hiyo ili ionekane kama ya kweli.

Zengwe la ndoa yao limebumbuluka hivi sasa baada ya viza ya miaka miwili aliyopewa Adenike kuisha na akiwa kwenye hatu za mwisho za kuomba sheria ya kuishi Uingereza milele.

Jelili na binti yake wanafanyiwa uchunguzi kuhusiana na tuhuma hizo na maafisa wa uhamiaji wa Uingereza wamesema kuwa ikithibitika kuwa tuhuma hizo ni za kweli basi Jelili na binti yake watapandishwa kizimbani na huenda wakatupwa jela kabla ya kurudishwa Nigeria.

http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3585118&&Cat=2
 
HAwa jamaa ni matapeli hata katika mahusiano!
 
Hii nayo kali. Lakini ni mbinu za kutafuta life. Angem 'do' ndio ingekuwa nongwa. Au kuna ushahidi labda walishamegana?
 
Msiwaseme wa Nigeria tu, The same shirt ina happen sana hata kwa Watanzania waishio nje.. !
 
Tongue Blizer,huwezi ukacompare large scale criminality ya Wanigeria na wa Tz ughaibuni.Ukiangalia prison za nchi zote za ulaya ,utakuta mnigeria.Serikali ya Uingereza inataka Kujenga gereza Nigeria ili kuwatransfer inmate wa Kinigeria wakaserve huko kwao!After Wajamaica,Wanigeria wanafuatia kwenye criminality.
Hata Thailand wako kwenye death row due to drugs.Watanzania hawajafika huko.
 


Nadhani mkuu nimeongelea katika issue hii ya ndoa za karatasi , Issue zingine ziwapelekazo prison Wanigeria siwezi ku comment kwasababu sina data zozote za wafungwa kwenye magereza ya nje.
 
Kupata makaratasi ,i agree,lakini baba na mtoto hii is above the norm.Sijasikia Mtz anafanya hivi
 
Kupata makaratasi ,i agree,lakini baba na mtoto hii is above the norm.Sijasikia Mtz anafanya hivi

Huwezi sikia kila kitu kama mimi ambavyo sijasikia kwamba Wanigeria ni namba 2 kwa Criminal duniani wakiongozwa na Wajamaica.
 
Wapo watu wanaofunga ndoa za namna hii hapa hapa Tanzania na hasa watumishi wa serkali kwa kisingizio cha kupata cheti cha ndoa na kuomba wahamie mjini kufuata waume zao feki.
 

Allegations: Jelili Adesanya insists Karimotu Adenike is his wife not his daughter

If they really are biologically unrelated as they claim, they should lend themselves to DNA testing and be able to prove one way or another that their marriage has been consummated.
 

Exactly how - by having an inbred offspring or a soft porn vid?! ha ha
 

Yeah, mwisho wa mambo yote ni DNA test. Maana kama ni binti yake huyu mzee amejipalia makaa ya moto kichwani mwake maana ulimwengu wa sasa si wa mwaka 47 ambapo mtu analiweza kubisha kitu kwa maneno lakini sasa hivi teknolojia iko kuondoa ubishi kama huu.
 
Kwa mtindo huu wanigeria wamepitiliza! Ukisoma hii habari unaweza kuhisi ni tamthilia fulani au movie za nollywood!
Kaoa binti kisa makaratasi ya kuishi uingereza? Mhh haya MAKARATASI mbona yanawapeleka pabaya!?
 
Kuna mwingine alio Mama yake! At the end of it, ikawalipukia, it is just pathetic.
 
Waungwana hivi katika sheria za dunia hii,(not bible) je imespecify kuwa wazazi na watoto wasioane.Just curious! jamaa asije kushinda kesi!
 

Dayyuuuum! He spit her out like no other. She is a female version of him.
 
Kwa mtindo huu wanigeria wamepitiliza! Ukisoma hii habari unaweza kuhisi ni tamthilia fulani au movie za nollywood!
Kaoa binti kisa makaratasi ya kuishi uingereza? Mhh haya MAKARATASI mbona yanawapeleka pabaya!?

Kuna mwingine alio Mama yake! At the end of it, ikawalipukia, it is just pathetic.

Yuko kijana mmoja yeye alimtanguliza mke wake kwenye nchi moja hapa Ulaya, huyu dada alipofika hapa akaolewa na mzungu na wakazaa naye binti mmoja ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 15. Baada ya kupata makaratasi huyu dada akaachana na mzungu na kwenda kumchukua mume wake huko Nigeria na kwa sasa wanaishi wote hapa na ni watu ninaowafahamiana nao kwa karibu. Sasa pigo walilopata ni kuwa baada ya hapo huyu dada hajafanikiwa kupata mtoto mwingine pamoja na juhudi za madaktari. Wanaigeria, mhhhhh! GOD forbid.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…