Afungiwa miezi 8 kutocheza mpira EPL

HIMARS

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Posts
70,791
Reaction score
98,334
Mshambuliaji wa Brentford Ivan Toney afungiwa kucheza, kushiriki mpira wa miguu kwa muda wa miezi 8 kuanzia leo pamoja na kulipa faini ya Tzs 150,000,000/

Hapo mwaka jana alikutwa na tuhuma za kucheza kamari, alishiriki kucheza kamari hadi kwenye mechi alizocheza wakati ni kinyume na sheria za mpira za Uingeleza ambazo haziruhusu Mchezaji wa Mpira kuanzia 5 tier kushiriki au kuhusika na kamari ya mpira
 
Ndo maana tunaliwa mikeka yetu kumbe mpuuzi anabet na uku Yuko uwanjan
 
Kwanza kuna haja gani ya kubeti wakati anakula mamilioni kila wiki!!

Kuna madaraja ya bets kulingana na kipato mkuu...

Mtu kama Drake pamoja na kuwa na hela huwa anapiga/pigwa mpunga kwa sababu ya kubet
 
Ivan toney
Granit Xhaka
Wote wamewahi kuwa na scandal ya kubet bookings ndo mana kwa kadi hawajambo
 
Alie mchoma ni rafiki yake, mi naamini hawa wachezaji wanabet ki siri sana bila mtu mwingine kujua. Toney alicho kosea ni kumshirikisha rafiki yake.
Ila jamaa bwege, angekuwa anampa mkeka mtu mwingine amchezee
 
Alie mchoma ni rafiki yake, mi naamini hawa wachezaji wanabet ki siri sana bila mtu mwingine kujua. Toney alicho kosea ni kumshirikisha rafiki yake.
Kuna yule jamaa wa trippier nae alimchoma kipindi anahama kwenda ATM
 
Amepigwa faini ya paundi 50,000.

FA ni wanafiki kwasababu wanaruhusu kampuni za betting kusponser team za mpira, matangazo kila kona halafu wanakataza wachezaji wasibeti,huu ni unafiki wa kiwango cha lami.

Ni sawa umweke mwanaume katika chumba kilichojaa wanawake walio uchi halafu umwambie ajizuie asidindishe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…