Afungwa jela kwa kuwapiga picha polisi wakikata roho

Afungwa jela kwa kuwapiga picha polisi wakikata roho

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Mwanaume mmoja nchini Australia amehukumiwa kifungo cha miezi 10 gerezani kwa kosa la kuwadhihaki na kuwapiga picha maafisa wa polisi wakati wakiwa wanakata roho katika ajali.

Mwezi uliopita Richard Pusey alikutwa na hatia katika shitaka ambalo si kawaida kutokea kwa kusababisha hasira kwa umma pamoja na makosa mengine. Mwanaume huyo mwenye miaka 42-tayari alikuwa kizuizini kwa siku 300 na anakaribia kumaliza muda wake.

Jaji aliyemuhukumu alisema, jambo aliliolifanya lilikuwa la kikatili na halikuwa na utu kabisa.
Bado familia za wahanga wa tukio hilo hawakuridhishwa na muda wa kifungo alichopewa na kuchochea hasira kubwa kwa umma.

Mwezi uliopita, Jaji Trevor Wraight alisema vyombo vya habari vimemtafsiri Pusey katika hali ambayo anaonekana kuwa mwanaume anayechukiwa zaidi nchini Australia.
 
Weka Picha au Video so alipokuwa anapiga picha alikuwa anacheka au why wakasirike hivyo? au hakutoa msaada?
 
Weka picha ya hao Mukora wakikata Roho.
 
Back
Top Bottom