Afungwa kwa kumnyonya ulimi mwanafunzi

kitalolo

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2006
Posts
1,827
Reaction score
708
na Walter Mguluchuma, Mpanda

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Mpanda imemuhukumu Kassim Lugendo (41) mkazi wa Kijiji cha Kambanga kifungo cha miaka 10 jela baada ya kupatikana na hatia ya kumnyonya ulimi msichana mwenye umri wa miaka 13, mwanafunzi wa darasa la tano katika Shule ya Msingi Igalula bila ridhaa yake.

Akitoa hukumu hiyo, Hakimu Mkazi Mfawidhi Chiganga Tengwa, alisema ametoa adhabu hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo.

Alisema ushahidi wa upande wa mashitaka na utetezi, umethibitisha kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo.

Akitoa utetezi wake kabla ya hukumu hiyo, mshitakiwa aliiomba mahakama isimpe adhabu kwa kile alichodai ana familia ya watoto saba na wazazi wake wote wawili ni walemavu na wanamtegemea yeye.

Pamoja na utetezi huo, hakimu Chiganga alisema kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha hatari, kwani kinaweza kikamsababishia msichana huyo kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi (VVU).

Awali, mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alidai mshitakiwa alitenda kosa hilo Machi 30 mwaka jana, majira ya saa 6 mchana akiwa nyumbani kwake.

Alidai siku hiyo msichana huyo akitoka shuleni akielekea nyumbani kwao, mshitakiwa alimuita na kisha kumwingiza kwa nguvu ndani ya nyumba yake na kumnyonya ulimi pamoja na kumwingiza vidole vyake sehemu za siri.

Alielendelea kudai kuwa wakati akimfanyia vitendo hivyo, msichana huyo alipiga mayowe na ndipo majirani wafika na kumkuta akifanya kitendo hicho huku sehemu ya sketi ya msichana huyo ikiwa imefunuliwa.

Source: Tanzania Daima
 
....dah!.....hivi mtu anaweza kumwaga kwa ulimi na kidole? Men tuache tamaa ya ngono kwani kama huna demu bafuni huwa unafanya nini? Its very simple, chukua picha ya Wema ibandike bafuni halafu anza kuoga huku unaiangalia
 
Kama mtu ana mke halafu anafanya upumbavu kama huu, nadhani huko anakoenda ndo mahala pake.
 
Nje ya mada kidogo. Hivi kujitetea kuwa nina majukumu mazito ya kifamilia, au nina wazazi wananitegemea inasaidia kweli?
 
Kama mtu ana mke halafu anafanya upumbavu kama huu, nadhani huko anakoenda ndo mahala pake.

Sio mke tu na watoto tena wa rika la huyo aliyemfanyia ushenzi
 
Nje ya mada kidogo. Hivi kujitetea kuwa nina majukumu mazito ya kifamilia, au nina wazazi wananitegemea inasaidia kweli?


Wala sio nnje ya mada mkuu huyu bwana kabla ya huo upuuzi alipaswa kulitambua hilo kuwa kama ana wazazi tena wagonjwa na watoto wengi wanomtgema basi alipaswa kujua kuwa jukumu lake katika jamii linampasa awe mtu mwenye kuheshimika katika jamii. Ingawa mara chache pia Mahakama huwa wanaangalia vitu kama hivyo huwa wanapunguza adhabu lakini kwa kutegemea na aina ya kosa
 
teh! maybe ruksa

Hana ruksa katika mazingira yoyote yale awe na mke na asiwe na mke kwani ameshindwa hata kuwatongoza mademu wamekaa wanasubiri kuto=ngozwa na kuliwa tu wewe unaenda kubaka?? eti kisa huna mke utaishia magereza
 
ukiziendekeza 'genye' ndio matokeo yake haya!

si matokeo ya bongo fleva,na tamthilia za malavi davi,,,ukipanda mchicha utavuna mchicha,,ndio jamii yetu ya sasa ,,,,aka,,,,kizazi,,,,cha,,malavi,,davi,,
 
Bila ridhaa?? .... Hata kama huyo binti angeridhia, bado ni statutory rape.
 
Nje ya mada kidogo. Hivi kujitetea kuwa nina majukumu mazito ya kifamilia, au nina wazazi wananitegemea inasaidia kweli?

ni jukumu la mahakama kama umemtia mtuhumiwa hatiani kabla hajajitetea kuomba huruma ya mahakama kabla ya kutamkwa adhabu(mitigating factors) na km mshtakiwa akipewa adhabu bla kupewa nafasi ya kuomba huruma ya mahakama basi anaweza kukata rufaa dhidi ya adhabu kuwa adhabu ilitolewa bila kufuata taratibu za kisheria(procedural irregularity) pia mtu akitoa 7bu nzr mahakama inaweza mpunguzia adhabu au hata kumwachia huru kbsa, eg, liumba aliiomba mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa alikuwa HIV+ na mahakama ikapunguza to two yrz
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…