Radam1
Member
- Aug 27, 2022
- 9
- 15
AFYA BORA KWA WATANZANIA:
Afya ni hali ya kuhisi/kujisikia vizuri kimwili pamoja na kiakili pia.Hivyo afya bora sio kula vizuri tu, bali hali nzuri yenye utulivu katika mwili na akili pia.Mwili wenye afya bora na njema huhitaji vitu kama vile mazoezi kiasi, muda wa mapumziko n.k. Yafuatayo ni mambo muhimu ya kuzingatia ili jamii iwe na afya bora;
Chanzo Cha picha: Muungwana BLOG
Usafi binafsi pamoja na mazingira, usafi umekuwa changamoto kubwa Sana katika jamii husika haswa kizazi cha sasa pasi na kutambua kuwa usafi ndiyo msingi muhimu wa kujikinga dhidi ya magonjwa hatarishi kama vile, kipindupindu ambacho hutokana na chakula kilichotayarishwa katika mazingira machafu na kuachwa wazi bila kufunikwa.
Hivyo hupelekea kushambuliwa na vijidudu vinavyosambaza ugonjwa huo kutoka Kwenye chakula hicho. Tunapaswa kuweka mazingira yetu safi bila kusahau miili yetu kujijali sisi wenyewe, angalau tuoge kutwa mara tatu kuondoa uchafu mwilini pamoja na harufu mbaya.
Chanzo cha picha: Muungwana BLOG
Kufanya mazoezi, mazoezi ni moja ya mambo muhimu sana ya kuzingatia katika afya yetu. Moja ya faida ni kutukinga dhidi ya magonjwa sugu na hatarishi yenye kutishia maisha yetu kama vile UVIKO-19 ambao hushambulia mifumo ya upumuaji yaani mapafu na hatimaye kusababisha mtu kushindwa kupumua vyema. Sasa basi kupitia mazoezi ya mwili, mifumo yote ile ya mwili
inayohusiana na upumuaji inaongezewa uwezo kufanya kazi vizuri katika miili yetu na hatimaye kudhoofisha virusi vya UVIKO-19 kushambulia mifumo hiyo.
Chanzo Cha picha: Mtanzania
Kupata lishe bora, jamii ifahamu
kuwa lishe bora ndio msingi wa afya. Sisi sote tunahitaji mlo kamili ambao unahusisha vyakula vyenye wanga kama vile mihogo, na viazi. Bila kusahau vyakula vyenye vitamini C kama vile machungwa na mananasi pamoja na vyakula vyenye protini kama vile samaki, mayai, na maharage kutaja kwa uchache. Lishe bora husaidia kuujenga mwili kwa kuufanya imara na wenye afya thabiti.
Kwahiyo ifahamike kuwa tunapaswa kula vyakula vinavyohitajika kwenye mwili na sio vinavyopatikana ilimradi tuwe tumekula la hasha! Kwa maana inaweza kuleta athari kubwa katika mmeng'enyo wa chakula na hatimaye mtu kupatwa na madhara Kama vile choo kigumu/kutoa kinyesi kigumu. Wakati kwa desturi na utaratibu wa mme'ngenyo tumboni Binadamu anatakiwa kupata choo angalau kutwa mara tatu. Ukiona hupati vile inavyotakiwa basi, kuna tatizo kwenye mfumo wa mmeng'enyo wa chakula kutokana na ulaji mbovu/usiofaa kwa wakati husika.
Kupata mapumziko, ikumbukwe kuwa kupumzisha miili yetu baada ya shughuli za kujitafutia ridhiki au labda baada ya kufanya kazi za nyumbani kwa muda mrefu inatupasa tupate muda muafaka wa kuituliza miili yetu pamoja na akili pia ili iweze kufanya kazi kwa ufasaha katika vipindi vijavyo.
Tabia ya kujiwekea ratiba ya kupumzisha miili yetu husaidia kuupa nafasi hata ubongo kuweza kutatua mambo yajayo kwa kina na kwa usahihi zaidi. Hivyo basi ili jamii iweze kuepukana na magonjwa mbalimbali inabidi kuweka swala la mapumziko kipaumbele.
Afya ni mtaji, bila ya afya hakuna maendeleo katika jamii. Hata ufanisi wa kufanya kazi mbalimbali hupungua kiwango kadri ambavyo afya inavyodhohofu. Zifuatazo ni athari ambazo jamii itapata endapo isipozingatia umuhimu wa afya;
Kuwa na mwonekano mbaya, mwili usio na afya njema hukosa mvuto. Sehemu kuu ya mwili ambayo huonesha muonekano huo ni ngozi. Ngozi ina nafasi kubwa katika miili yetu, ngozi ikiwa imeharibika kwa kutozingatia usafi binafsi ili iwe na afya njema na kuvutia basi mtu anaweza kuonekana mzee zaidi kabla ya umri wake.
Kukosa kujiamini, mtu asiyekuwa na afya hukosa kujiamini na huwaza mawazo hasi katika maisha yake, huona kama vile amepoteza mwelekeo na kujiona kila kitu hawezi ingalikuwa uwezo anao wa kujitosheleza ili kufikia hatima yake. Tunapokuwa na afya njema hata ubongo hutafsiri hiyo hali na hatimaye kuipa nguvu miili yetu kufanya kazi inayotukabili au itakayotukabili kwa kujiamini zaidi bila wasiwasi wowote.
Kukosa matumaini, afya ikiwa mgogoro tunaweza kosa matumaini ya kuishi na kufika malengo ambayo tumekusudia. Mfano mtu aliyeathirika na magonjwa sugu kama vile kansa ya koo, homa ya ini, kutaja kwa uchache. Mtu kama huyo hawezi kuona ya fursa ya kuishi tena kutokana na afya yake kuwa mgogoro.
Kunyemelewa na magonjwa, miongoni mwa athari za kutozingatia afya zetu ni kunyemelewa kiurahisi na magonjwa hatarishi.Yaani kinga ya mwili hushuka na kuyapa nafasi magonjwa mengine kuingia kama vile, kifua kikuu, maambukizi kwenye kibofu cha mkojo n.k.
Kwa kumalizia, swala la afya bora ni letu sote watanzania ingalikuwa pongezi nyingi sana zitangulie kwa serikali yetu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania dhidi ya uhamasishaji wa kunawa mikono yetu kwa maji safi na sabuni ili kutulinda dhidi ya magonjwa hatarishi kama vile UVIKO-19 ambao umekuwa ukileta hofu katika jamii. Hapa juhudi ya serikali inaonekana baada ya Tanzania kupokea dozi 1,058,400 za chanjo ya UVIKO-19 kutoka nchini Marekani mnamo tarehe 24 julai 2021.
Chanzo Cha picha: Mwananchi
Na bado ikasisitiza tuvae barakoa sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa watu wengi Kama vile mashuleni, sokoni, n.k. Ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo hatarishi katika
nchi yetu.
Chanzo Cha picha: Health Studio
Hii inaonesha dhahiri kuwa nasi watanzania tujaribu kuwekea mkazo swala la Afya kwa kushirikiana na serikali yetu ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Bila kusahau kuonyana kwa vitendo pale ambapo tunaona ndugu,jamaa, rafiki au jamii husika inapokiuka umuhimu wa afya bora ili kusaidia vizazi vingine vijavyo. Kwa pamoja tunaweza!

Upvote
105