JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Kung’ata kucha(Onychophagia)
Tabia ya Kung’ata kucha inaweza kuwa haina madhara iwapo itakuwa ya muda labda wasiwasi wa urembo wa kucha lakini tabia hii inaweza kuendelea na kulifanya tatizo la kudumu. Kung’ata kucha kulikopitiliza(Onychophagia) kunaharibu kucha na tishu zilizozizunguka
DALILI
Kung’ata kucha kulikopitiliza(Onychophagia) ambayo matokeo yake ni kuharibu kucha inaweza kuambatana na tabia nyingine zinazofanana kwenye mwili kama kuvuta nywele au kuvuta ngozi. Watu wanaong’ata kucha inaweza kuwa wanapitia
• Hisia za hofu kabla ya kung’ata kucha
• Kuhisi vizuri au raha baada ya kung’ata kucha
• Hisia za aibu,kudhalilika vikihusiana na muonekano wa ngozi na kucha vinavyosababishwa na kung’ata kucha
• Uharibifu wa tishu za vidole na kucha
• Vidonda mdomoni, matatizo ya kinywa, majipu na maambukizi
• Kwa baadhi, kung’ata kucha kulikopitiliza kunaweza kusababisha matatizo ya kifamilia na kijamii
Kwa kawaida kun’gata kucha huanzia utotoni na inaweza kundelea mpaka utu uzima japokuwa tabia hii hupungua au kuacha kulingana na umri
SABABU
Baadhi ya watu wanaweza kurithi pia kiwango kikubwa cha mhemko na wasiwasi vinaweza kusababisha. Kung’ata kucha inahusiana na wasiwasi kwa sababu kitendo cha kung’ata kucha kinatajwa kupunguza hofu au kuondoa kuboreka.
Watu wanaong’ata kucha wameelezea kufanya hivyo iwapo wanahisi wasiwasi, kuboreka, upweke au hata njaa
MATIBABU
Tiba ya kuweka kitu kichungu au kinachowasha kwenye vidole imeonekana kutofanya kazi. Kuzuia kwa kuziziba kucha kama kutumia glovu na soksi vinaweza kutumika kama vizuizi vya kung’ata kucha au ukumbusho wa kutong’ata. Matibabu kwenye tabia iliyopitiliza pia inatakiwa ilenge kuondoa hisia zinazopelekea kung’ata kucha