Emerald Maggie
New Member
- Jul 26, 2021
- 1
- 0
AFYA
Ni hali ya mtu kua mzima kimwili, kijamii na kiakili. Uzima wa mtu katika nyanja zote una mchango mkubwa juu ya mwenendo wa maisha na maamuzi ya mtu katika nyakati mbalimbali.
Uzima wa kimwili humwezesha mtu kufanya kazi na kutimiza majukumu yake ya kila siku na hivyo kujiendeleza kijamii, kiuchumi, kitaaluma na kiroho. Afya ya mwili ni mhimili mkubwa sana wa maisha ya binadamu yeyote.
MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUWA NA AFYA BORA YA MWILI.
Afya ya akili inahusisha hisia, saikolojia ya mtu na vile anavyoshinda mkazo na madhara yake.
Mambo ya kufanya:
Endapo mtu anaishi mahali pasafi na mazingira yanayomzunguka ni masafi na hakuna magonjwa, atakua na afya bora kuliko ambavyo angekua endapo mazingira yangekua machafu. Mazingira machafu husababisha magonjwa hivyo afya ya mwili na akili kudhoofu.
KIPATO CHA MTU.
Kipato cha mtu huchangia mtu kupata mahitaji yake ya muhimu kwa wakati muafaka. Mtu mwenye kipato kizuri ni rahisi kutimiza mahitaji yake kama chakula, mavazi, malazi na matibabu pale anapougua hivyo kua na afya bora.
Kipato duni hufanya mtu ashindwe kupata mlo kamili na matibabu anapougua hivyo kua na afya duni kimwili na kiakili na hatimaye hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
KIWANGO CHA ELIMU
Elimu humwezesha mtu kufanya maamuzi sahihi katika nyakati mbalimbali hasa penye changamoto au jambo lenye utata. Mtu anapokua ameelimika ni rahisi sana kujali afya yake na kuzingatia kanuni za afya bora ya mwili na akili. Wakati mwingine ukosefu wa elimu ya afya husababisha watu kufanya mambo yanayohatarisha afya bila tahadhari na hivyo kudhoofisha mwili.
Mtu aliyeelimika anajua kuwa AFYA NI MTAJI na anajali afya yake muda wote.
MILA NA DESTURI ZA JAMII HUSIKA
Baadhi ya mila na desturi huwa zinakwenda kinyume na uchochezi wa afya bora na husababisha magonjwa kuenea kwa watu. Mila kama za ukeketaji wa watoto wa kike; hii huharibu afya ya mwili na husababisha hitilafu kwa mtu hasa kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho ni hatari na huambatana na maumivu makali.
Pia baadhi ya mila na desturi hukataza ulaji wa baadhi ya vyakula ambavyo vina umuhimu na huleta afya bora. Hivyo kwa asilimia kubwa husababisha udhoofu wa mwili na kupunguza ufanisi wa akili.
AJIRA NA UKOSEFU WA AJIRA
Ajira ni kazi halali afanyayo mtu ili kupata kipato na kukidhi mahitaji yake na ya wale wanaomtegemea.
Ukosefu wa ajira hupelekea watu kushindwa kumudu mlo kamili na hivyo kutokua na afya bora. Pia ukosefu wa ajira husababisha watu wengi kushindwa kuhimili gharama za matibabu. Pia hupelekea watu kuishi maisha duni na maeneo yenye hatari ya maambukizi ya magonjwa hasa ya mlipuko kama kipindupindu na hivyo afya kutetereka.
GENETICS
Baadhi ya watu wanazaliwa wakiwa na hali mbalimbali zinazowafanya kuwa katika hatari ya kupata magonjwa au kua na afya duni. Pia watu wengine huzaliwa na hitilafu za ndani na husababisha kua na hali duni kisaikolojia hivyo kua na afya duni ya akili muda wote.
USHAURI WA NAMNA YA KUBORESHA AFYA YA MWILI NA AKILI KWA UJUMLA
AFYA NI BORA KULIKO MALI.

- Kuzingatia usafi na unadhifu wa mwili na usafi wa mazingira muda wote.
- Kula mlo kamili na vyakula bora ili kuupa mwili nguvu na kujikinga na magonjwa, kwa kula matunda, maji, madinijoto na vyakula vya wanga na protini.
- Kupunguza au kuepuka utumiaji wa pombe na sigara au kemikali zozote zenye madhara kwenye miili yetu.
- Kuzingatia chanjo za magonjwa mbalimbali na kujikinga na magonjwa hasa ya kuambukizwa.
- Kufanya mazoezi mara kwa mara ili kuimarisha kinga ya mwili na kuwa wakakamavu.
- Kuchukua tahadhari hasa wakati wa kutumia vyombo vya moto kama magari na pikipiki na vifaa vyenye ncha kali au mambo mbalimbali yanayotuweka kwenye hatari kiafya.
Afya ya akili inahusisha hisia, saikolojia ya mtu na vile anavyoshinda mkazo na madhara yake.
Mambo ya kufanya:
- Furahia maisha kama zawadi uliyopewa na Mungu .
- Weka mlinganyo wa maisha katika nyanja za uchumi, familia na imani.
- Jifunze kushinda majaribu na kila baada ya anguko au matatizo tafuta tumaini jipya.
- Jifunze kuzoea hali zote za maisha hasa changamoto kwa kutumia mbinu ili kukabili changamoto hizo.
- Wakati mwingine soma vitabu mbalimbali vya kuhamasisha mwenendo chanya wa maisha, kama vitabu vya dini, na machapisho ya waandishi mbalimbali kuhusu maisha, mafanikio, changamoto, imani, upendo na maendeleo.
- Mazingira anayoishi na yale yanayomzunguka.
- Mila na desturi za jamii husika.
- Kiwango cha elimu .
- Kipato cha mtu, hali ya uchumi.
- Hali ya ajira.
- Hali ya muundo wa genes
Endapo mtu anaishi mahali pasafi na mazingira yanayomzunguka ni masafi na hakuna magonjwa, atakua na afya bora kuliko ambavyo angekua endapo mazingira yangekua machafu. Mazingira machafu husababisha magonjwa hivyo afya ya mwili na akili kudhoofu.
KIPATO CHA MTU.
Kipato cha mtu huchangia mtu kupata mahitaji yake ya muhimu kwa wakati muafaka. Mtu mwenye kipato kizuri ni rahisi kutimiza mahitaji yake kama chakula, mavazi, malazi na matibabu pale anapougua hivyo kua na afya bora.
Kipato duni hufanya mtu ashindwe kupata mlo kamili na matibabu anapougua hivyo kua na afya duni kimwili na kiakili na hatimaye hushindwa kufanya kazi kwa ufanisi.
KIWANGO CHA ELIMU
Elimu humwezesha mtu kufanya maamuzi sahihi katika nyakati mbalimbali hasa penye changamoto au jambo lenye utata. Mtu anapokua ameelimika ni rahisi sana kujali afya yake na kuzingatia kanuni za afya bora ya mwili na akili. Wakati mwingine ukosefu wa elimu ya afya husababisha watu kufanya mambo yanayohatarisha afya bila tahadhari na hivyo kudhoofisha mwili.
Mtu aliyeelimika anajua kuwa AFYA NI MTAJI na anajali afya yake muda wote.
MILA NA DESTURI ZA JAMII HUSIKA
Baadhi ya mila na desturi huwa zinakwenda kinyume na uchochezi wa afya bora na husababisha magonjwa kuenea kwa watu. Mila kama za ukeketaji wa watoto wa kike; hii huharibu afya ya mwili na husababisha hitilafu kwa mtu hasa kwa kuzingatia kuwa kitendo hicho ni hatari na huambatana na maumivu makali.
Pia baadhi ya mila na desturi hukataza ulaji wa baadhi ya vyakula ambavyo vina umuhimu na huleta afya bora. Hivyo kwa asilimia kubwa husababisha udhoofu wa mwili na kupunguza ufanisi wa akili.
AJIRA NA UKOSEFU WA AJIRA
Ajira ni kazi halali afanyayo mtu ili kupata kipato na kukidhi mahitaji yake na ya wale wanaomtegemea.
Ukosefu wa ajira hupelekea watu kushindwa kumudu mlo kamili na hivyo kutokua na afya bora. Pia ukosefu wa ajira husababisha watu wengi kushindwa kuhimili gharama za matibabu. Pia hupelekea watu kuishi maisha duni na maeneo yenye hatari ya maambukizi ya magonjwa hasa ya mlipuko kama kipindupindu na hivyo afya kutetereka.
GENETICS
Baadhi ya watu wanazaliwa wakiwa na hali mbalimbali zinazowafanya kuwa katika hatari ya kupata magonjwa au kua na afya duni. Pia watu wengine huzaliwa na hitilafu za ndani na husababisha kua na hali duni kisaikolojia hivyo kua na afya duni ya akili muda wote.
USHAURI WA NAMNA YA KUBORESHA AFYA YA MWILI NA AKILI KWA UJUMLA
- Jifunze kumudu hofu na mkazo ili kuishi kwa amani na furaha; hii husaidia pia kujikinga na magonjwa ya moyo.
- Tumia muda wa japo dakika kumi na tano au thelathini kwa ajili ya kufanya mazoezi ya mwili. Hii husaidia kuboresha afya ya viungo na mwili. Pia mazoezi huboresha afya ya akili na kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kama mafua na magonjwa ya moyo.
- Kula mlo kamili wenye virutubisho kama vitamini, wanga, mafuta, madinijoto, na protini. Pia kunywa maji ya kutosha angalau lita tatu kwa siku ili kuimarisha afya ya figo.
- Kujenga mazoea ya kwenda hospitali mara kwa mara kwa ajili ya kuchunguza afya na kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari na shinikizo la damu (presha), kwani TAHADHARI NI BORA KULIKO TIBA NA USIPOZIBA UFA UTAJENGA UKUTA. Pia kwenda hospitali muda punde unapohisi unaumwa au unapopata ajali au tatizo lolote kiafya ili kupata matibabu na kuepuka athari zaidi.
- Ishi na watu vizuri ili kupunguza ugomvi na madhara yake, hasa majeraha na hatari za kimwili na kiakili, jali watu na pia kua karibu na wale wanaokujali, hii itakuongezea furaha na hamasa ya kutenda mambo mema.
- Ishi kwa kufuata mwenendo mzuri wa maisha, epuka matumizi yaliyopitiliza ya pombe na sigara kwani huharibu viungo vya mwili na kudhoofisha kinga ya mwili, apuka vyakula vyenye sukari nyingi ili kuweka sawa kiasi cha sukari mwilini.
- Jihusishe na kazi halali ili kujipatia kipato na kutimiza mahitaji binafsi na ya wale wanaokutegemea.
- Fuata mafundisho ya dini na mambo yote yanayohimiza mahusiano mema na watu ili kupunguza ugomvi na mkazo utokanao na chuki.
AFYA NI BORA KULIKO MALI.
Upvote
0