SoC04 Afya na maabara

SoC04 Afya na maabara

Tanzania Tuitakayo competition threads

Aweking

New Member
Joined
Mar 10, 2019
Posts
4
Reaction score
0
UTANGULIZI
Katika sekta ya afya kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa vipimo vya awali katika zahanati za serikali , hii hali inapelekea vifo au hali hatarishi zaidi kwa zile jamii ambavyo vipo mbali na vituo vya afya ,hospitali au hospitali za rufaa ..

MAADA NA MAELEZO KAMILI
Tanzania tumepiga hatua kuanzishwa kwa zahanati kila kijiji ,tatzo kubwa ni kuwa maabara hizo hazina maabara kwa ajili ya vipimo vya awali mfano HB ( kujua uwingi w damu)RBG/FBG (kujua kiwango cha sukari kwenye damu)
Zahanati za serikali kutokuwa na maabara kwa ajili ya hivyo vipimo pamoja vipimo vingine vya awali inahatarisha maisha ya watanzania wengi.

Zahanati binafsi zinakuwa na hizo vipimo vya awali kwanini zahanati za serikali hazina?

Zahanati za serikali vipimo vinavyopatikana ni HIV, MRDT , vipimo hivyo hufanyika kwenye meza ya daktari..

MAPENDEKEZO
1. Serikali iimarishe huduma za maabara katika zahanati za serikali.
2. Serikali ifanye uboreshaji wa huduma hitajika za maabara ngazi ya zahanati
3. Serikali iangalie ushindani wa Ki maabara katika zahanati za serikali na binafsi.

MAPENDEKEZO YA VIPIMO VINAVYOTAKIWA VIPATIKANE KATIKA ZAHANATI ZA SERIKALI.
1. MRDT
2. Urinalysis
3. Stool analysis
4. RBG/FBG
5. HB/HGB
6. RPR/VDRL
7. PITC/HIV
8. WIDAL TEST

FAIDA ZA VIPIMO HIVYO
1. Itasaidia jamii kujua tatzo mapema
2. Itapunguza gharama za matibabu
3. Itapunguza vifo kama vile wanawake wajawazito wanaopata upungufu wa damu , mtu kushuka kiwango cha sukari mwilini .
4. Itaongeza nafasi za ajira kwa wataalamu wa maabara.
5. Itasaidia jamii nyingi kugundua ugonjwa, na kama haina uwezo wa kutibika katika ngazi ya zahanati basi itapewa rufa mapema ili lipate kutibika.

MAONO YANGU
Serikali iwe na sera dhabiti kuanzishwa kwa maabara kwa kila zahanati ya serikali hili wazo linaweza tekelezeka ndani ya miaka 5 !!
 
Upvote 2
Zahanati za serikali kutokuwa na maabara kwa ajili ya hivyo vipimo pamoja vipimo vingine vya awali inahatarisha maisha ya watanzania wengi
Jamani, mbona ni masikitiko yaani, inamaana magonjwa wanatumia ramli ama nn?

Serikali iwe na sera dhabiti kuanzishwa kwa maabara kwa kila zahanati ya serikali
Nakubali, vipimo vya msingi ndo hivyo.... ni vya MSINGI
 
Back
Top Bottom